Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema migogoro mingi ya ardhi mkoani Arusha inachochewa na uzembe wa viongozi katika mabaraza ya ardhi pamoja na mahakama kutokutimiza wajibu wao ipasavyo.Kauli hiyo ameotoa wakati wa mkutano na wananchi wa wilaya ya Karatu wenye kero mbalimbali za ardhi, Nyumba na Makazi.
"Toka nianze mikutano hii na wakazi Arusha na leo nipo hapa Karatu migogoro mingi si mikubwa kama inavyoonekana bali inachangiwa na uzembe wa watu wetu katika mabaraza ya ardhi na mahakama kutokutimiza wajibu wao ipasavyo" Gambo.
Vilevile amemuagiza Kamishna wa ardhi kutuma timu maalum itakayoshughulikia kero hizo ndani ya muda mfupi na kuyafanyia ukaguzi mabaraza yote ya Ardhi wilaya za Arusha mjini na Karatu.
“Kamishna nitakutana mara baada ya ziara ya mwenge kupita mkoani mwetu ulete timu maalum itakayopiga kambi hapa kumaliza kero hizi kwani hapa kuna wengine wala hawana migogoro ya ardhi bali wamevamiwa kwenye maeneo yao watu kama hawa polisi ndiyo sehemu husika na sio kwenye mabaraza ya ardhi, vilevile ukayafanyie ukaguzi mabaraza ya Ardhi ya Arusha mjini na Karatu kwani nayo sioni kama wanafanya kazi zao sahihi sana”
No comments:
Post a Comment