MBEKI: WAKENYA WAMERIDHIA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU

ALIYEKUWA Rais wa pili wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amesema kuwa wananchi wamepokea na kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu waangalizi wa kimataifa walio hapa Kenya kushuhudia uchaguzi mkuu wa Jumanne Agosti 8, 2017.

Mbeki anayeongoza ujumbe kutoka bara la Afrika akihutubia waandishi wa habari Ijumaa katika hoteli ya Crowne Plaza jijini Nairobi, amesema kuwa utangamano wa wachunguzi wa AU wapatao 104 na wananchi, umefichua Wakenya wanataka shughuli ya uchaguzi uwe wa huru, haki na wazi.

"Wakenya ambao tumeongea nao wametukaribisha kwa dhati na kufurahishwa na ziara yetu, wamesema ni vyema tuchunguze uhalisia wa uchaguzi wakihoji wanataka uchaguzi wa huru, haki na wazi," amesema Mbeki.

Katibu huyu ameongoza zaidi ya wachunguzi 5,000 wa hapa Kenya, kimataifa, wa uchaguzi huo wakiwemo waandishi wa habari nchini na dira tofauti za dunia.

"Wajibu wetu ni kuchunguza na kuandika ripoti ya shughuli hiyo ya uchaguzi," akasema Bw Mbeki.

Akaongeza: "Hatutaona mambo yakienda vibaya tunyamaze, na ifahamike vyema kwamba hatutaandika ripoti nzuri iwapo matukio yataenda kinyume na inavyotarajiwa."

Kando na Bw Mbeki, wachunguzi wengine wa kimataifa ni: Katibu Mkuu wa Marekani John Kerry, Rais Mstaafu wa Ghana John Dramani Mahama, Katibu Mkuu wa muungano wa Commonhealth Bi Patricia Scotland, miongoni mwa wengine.

Uchaguzi ujao unatarajiwa kutifuka kivumbi kati ya farasi wawili ambao ni Rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee na kinara wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) Mheshimiwa Raila Odinga.

Asasi inayosimamia uchaguzi Kenya ni tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Bw Wafula Chebukati.

MBEKI: WAKENYA WAMERIDHIA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU MBEKI: WAKENYA WAMERIDHIA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU


Reviewed by KUSAGANEWS on August 04, 2017 Rating: 5

No comments: