WANAWAKE WA ARUSHA WAOMBA ENEO MAALUM KWA AJILI YA KUTANGAZA UTALII WA NDANI


Katikati ni Mgeni Rasmi katika tamasha akikabidhiwa zawadi maalum kwa jina la LOSHORO


Mgeni rasmi akizungumza na akina mama
Mwanzilishi wa Tamasha la MWANAMKE WA AFRIKA Bi Amina TEMAMBELE AKITOA NENO LA SHUKRANI
Wanawake wajasiriamali katika jiji la Arusha Wameomba serikali iwapatie eneo maalum kwa ajili ya kuwakutanisha wanawake wajasiriamali kwa pamoja kwa ajili ya  biashara zao ili wageni wanapotembelea Arusha watambue eneo la bidhaa zinazotengenezwa na mwanamke wa Afrika.

Akizungumza katika Tamasha la wanawake wajasiriamali Jijini Arusha Mgeni Rasmi Bi Anna Msuya kwa niaba ya Violeth Semfuko amesema kuwa ni wakati wa Mwanamke wa Afrika kuamka na kutambua kuwa zipo fursa kimataifa kwa kufanya ujasiriamali.

Bi Ana amesema kuwa wanawake wakichangamkia fursa zilizopo suala la kuwezeshwa baadae litakuwa halipo na kuwataka wanawake wa arusha Kufanya jambo hilo kuwa endelevu kila mwaka ili kumsaidia mwanamke kujkwamua na umasikini.
 
Awali akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi katika tamasha hilo Lidya Mapunda amesema kuwa kauli mbiu ya Tamasha hilo la wanawake wajasiriamali ni AMKA MWANAMKE na wamepanga kufanya tamasha hilo kiola mwaka na kuwakutanisha wanawake na wadau mbalimbali hasa katikia sekta ya utalii.

Kwa upande wake mkurugenzi aliyefanikisha tamasha hilo Bi AMINA TEMAMBELE ameiomba serikali kuendelea kuunga mkono wanawake ambao wana lengo la kujikwamua na umaskini ambapo katika mwaka ujao watafanya maandalizi ya kutosha ili kufanikisha zoezi hilo endelevu. 
WANAWAKE WA ARUSHA WAOMBA ENEO MAALUM KWA AJILI YA KUTANGAZA UTALII WA NDANI WANAWAKE WA ARUSHA WAOMBA ENEO MAALUM KWA AJILI YA KUTANGAZA UTALII WA NDANI Reviewed by KUSAGANEWS on July 08, 2017 Rating: 5

No comments: