Wanafunzi Majeruhi wa ajali ya lucky Vincent waliopo marekani kwa matibabu kurejea nchini mwezi ujao.

Wanafunzi watatu wa shule ya Lucky Vincent ambao walijeruhiwa katika ajali iliyotokea Mei 6  mwaka huu na kuuwa wanafunzi  32 walimu wawili na dereva wanatarajia kurejea nchini mwezi ujao.

Wanafunzi hao,Wilson Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh,waliondoka nchini na kufika Marekani Mei 15,kwa matibabu katika hospitali ya Mercy  nchini Marekani.

Katika taarifa ya Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu amesema kuwa wanafunzi hao, watarejea na wazazi wao na madaktari waliowasindikiza kwa ajili ya matibabu.

"Tunapanga kuwarejesha nyumbani watoto Wilson, Doreen na Sadia pamoja na wazazi wao , mwezi ujao pamoja naa Dkt. Elias Mashalla na Muuguzi wa Mount Meru hospital watasafiri pamoja na watoto kurudi, kama walivyoondoka"alisema

Nyalandu amesema  kwa sasa, Mtoto Doreen anatarajiwa kwenda Kituo cha Madonna, Nebraska baada ya miadi yake ya mwisho ya kuonana na Dkt. Steve Meyer, Julai 10 kutokana matibabu ambayo alikuwa anapata..

Amesema Doreen ambaye ndiye alikuwa na majeraha makubwa katika ajali hiyo, anatarajiwa kukaa katika kituo hicho mahususi kwa Mazoezi ya Uti wa mgongo  kwa wiki 4..

Nyarandu ambaye ndiye amefanikisha safari na matibabu ya watoto hao nchini Marekani amesema  Watoto Sadia na Wilson wataendelea kukaa katika kituo cha Mc Donald, Sioux City IA hadi watakapokuwa tayari kwa safari.

"Wikiendi hii tunakamilisha taratibu za safari na namna watakavyo safari na nategemea kutoa Taarifa kamili kufikia Jumanne wiki ijayo"alisema

Wanafunzi hao, walinusurika katika ajali hiyo iliyouawa watu 35,, iliyotokea Mei 6 wakiwa safarini, kutoka Arusha kuelekea Karatu katika shule ya Tumaini kufanya mitihani ya ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wamepanda kuanguka katika korongo eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Wanafunzi Majeruhi wa ajali ya lucky Vincent waliopo marekani kwa matibabu kurejea nchini mwezi ujao. Wanafunzi Majeruhi wa ajali ya lucky Vincent  waliopo marekani kwa matibabu kurejea nchini mwezi ujao. Reviewed by KUSAGANEWS on July 08, 2017 Rating: 5

No comments: