Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji nchini kuondoa hofu kwani kamati ya pili iliyoundwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.
Majaliwa amebainisha hayo leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka aliyetaka kujua hatma ya zuio la usafirishaji wa makinikia hayo.
"Mpaka
sasa tumepokea taarifa moja na bado tunasubiri taarifa ya pili katika hili
nataka niwasii wawekezaji wote kwanza wasiwe na mashaka kwa sababu lengo la
serikali ni kujiridhisha tu kwamba je mchanga huu unaosafirishwa kwenda nje una
nini na hatu bugudhi uzalishaji wao. Baada ya kuwa tumepata ile taarifa ya
kwanza bado hatua kamili hazijachukuliwa tunasubiri taarifa ya kamati ya pili
baada ya hapo sasa serikali itaka chini na kutafakali kwa kupata ushauri kutoka
sekta mbalimbali za kisheria, kiuchumi na maeneo mengine hatua gani tuchukue
kwa hiyo nitoe rai hata kwa watanzania wawe watulivu wasuburi majibu ya
serikali ambayo yatalinda haki ya kila muwekezaji" alisema Majaliwa.
Uchunguzi makinikia haujakamilika - Majaliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment