Mzee Ngosha hakuwa mbunifu - Wambura



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa marehemu Mzee Francis Kanyasu hakuwa mbunifu wa nembo ya taifa kama watu wanavyodhania bali alikuwa mchoraji.

Wambura amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Devotha Minja alilouliza juu ya serikali kushindwa kumthamini pamoja na kumuhujumu Mzee Ngosha aliyechora nembo ya taifa na hatimaye kufa masikini.

Waziri Wambura amesema  kuwa Si kweli kwamba Mzee Ngosha serikali imemuhujumu, bali yapo majina mezani kama matatu yanayohusiana na ubunifu wa nembo ambayo inatumika kama, nembo ya taifa. 

Ameongeza kuwa mpaka sasa bado haijajulikana nani hasa ambaye ni mbunifu wa nembo hiyo  kwa sababu yupo marehemu ambaye alishatangulia mbele za haki muda mrefu ambaye anaitwa Abdallah Farhani wa Zanzibar yeye vielelezo tayari vishakutwa katika kumbukumbu zake jinsi alivyokuwa akibuni nembo ya taifa, nembo ya Kenya pamoja na hata nembo ya OAU kipindi hicho alipokuwa anasoma Makerere University.

Pamoja na hayo Naibu Waziri amewaomba wataalamu kufuatilia kiundani kabisa juu ya suala hili ili waweze kutambua ukweli wake.
Mzee Ngosha hakuwa mbunifu - Wambura Mzee Ngosha hakuwa mbunifu - Wambura Reviewed by KUSAGANEWS on June 01, 2017 Rating: 5

No comments: