MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA ATHUMANI KIHAMIA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABISHARA ULIOFURUKUTA KWA MUDA MREFU




Mkurugenzi wa jiji la Arusha akizungumza na wafanyabiashara
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amemaliza rasmi mgogoro uliokuwa umedumu kwa muda mrefu baina ya wafanyabiashara Wajenzi pamoja na wafanyabiashara wapangaji katika halmashauri hiyo ya jiji la Arusha.

Akizungumza na wafanyabiashara hao wa pande zote mbili kihamia Amesema kuwa mgogoro huo umeisha na makubaliano ni kwamba baina ya vikao vya madiwani ni kuwa wajenzi hawajamalizana na halmashauri hivyo wataendelea kumiliki vibanda hivyo mpaka hapo maelekezo mengine yatakapotolewa.

”””Katika kuona tuwasaidieje nimeongea na pande zote mbili kwa vipindi tofauti kuna makubaliano maalum ambayo tumekubaliana kila upande lakini na kuyaleta pamoja na kwasasa hivi nayatangaza kama ifuatavyo mbele yao kubaliano namba moja ni namna ambavyo kodi italipwa kwamba kwa kuwa wajenzi wamejenga vibanda na jiji hawajamalizana nao mana ake ni wazi kwamba wanamiliki bado vibanda na tumekubaliana tuwape mikataba ya muda mrefu hii ni kwa mujibu wa kikao cha kamati ya madfiwani”””

Kihamia amesema hayo yamekuja baada ya vikao mbalimbali vya baraza,pamoja na vikao vya kamati ya fedha vinavyohusisha madiwani na makubaliano yao ni kuwa mfanyabiashara ambaye ni mpangaji atalipa kodi kwa mfanyabiashara mjenzi na mjenzi atalipa halmashauri kwa mujibu wa mkataba ambao wameingia ili kutatua jambo hilo na lifikie mwisho.

Pia amesema kuwa yeye kama  mkurugenzi kwa muda mrefu amewashawishi wafanyabiashara mpaka wametoa kesi iliyokuwepo mahakamani lengo ni ili kuona watakavyo maliza mgogoro huo na sasa amewashukuru kwa kukubaliana ili kuendelea kujenga jiji la Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wapangaji Josephine Esuphat wamemshukuru mkurugenzi Kihamia kwa kuwa suala hilo huenda lingeleta matatizo baina yao na wamepata moyo na serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali wafanyabiashara hao.

Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Bwana Lokeni Adolf Masawe amesema amemshukuru mkurugenzi kwa kujali pande zote mbili ambazo zilikuwa na mgogor.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA ATHUMANI KIHAMIA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABISHARA ULIOFURUKUTA KWA MUDA MREFU MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA ATHUMANI KIHAMIA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABISHARA ULIOFURUKUTA KWA MUDA MREFU Reviewed by KUSAGANEWS on June 03, 2017 Rating: 5

No comments: