Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) imewasilisha bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2017/18 ikiomba
kuidhinishiwa Sh6.5 trilioni huku kiasi kikubwa cha fedha Sh 4.07 trilioni
zikienda kwenye mishahara
Bajeti hiyo iliwasilishwa na Waziri wa Tamisemi, George
Simbachawene aliyesema kuwa kati ya fedha hizo, Sh4.54 trilioni zitatumika
katika matumizi ya kawaida (mishahara na matumizi mengineyo).
Kwa mujibu wa bajeti hiyo Sh1.78 trilioni zinaombwa katika
kugharamia miradi ya maendeleo
Wakati Tamisemi ikiomba fedha hizo, mwaka 2016/17 Bunge
liliidhinisha Sh6.02 trilioni huku mishahara ikitafuna Sh3.7 trilioni, sawa na
theluthi mbili ya bajeti, na Sh1.6 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hata hivyo, hadi kufikia Februari mwaka huu (miezi minne
kabla ya mwaka wa bajeti kumalizika), fedha zilizopokelewa na wizara hiyo
zilikuwa ni Sh3.55 trilioni (Sawa na asilimia 59.1) ya bajeti yote
iliyoidhinishwa na Bunge
Watumishi hewa
Simbachawene alisema watumishi 13,369 ambao ni watoro na
waliofariki dunia wameondolewa katika orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali
Alisema kati ya idadi hiyo, 541 walikuwa ni wa sekretarieti
za mikoa na watumishi wa serikali za mitaa ni 12,828 ambao waliisababishia
Serikali hasara ya Sh25.4 bilioni
Hata hivyo, alisema Sh 2.7 bilioni sawa na asilimia 11
zimerejeshwa serikalini
Ufuatiliaji unaendelea ili kuhakikisha fedha zilizobaki
zinarejeshwa na kuwachukulia hatua watumishi waliohusika na upotevu huo,”
alisema Simbachawene
Alisema watumishi wasio waadilifu wameendelea kuchukuliwa
hatua
Elimu bila malipo
Kuhusu suala la elimu bure, Simbachawene alisema kuna
tofauti kati ya elimu bure ya msingi na elimu ya msingi bila malipo
Wananchi wanakuwa wazito kujitolea hata nguvu zao katika
kuchangia shughuli mbalimbali zinazohusu elimu kwa kisingizio kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inatoa elimu msingi bure,” alisema
Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wabunge, wakuu wa mikoa,
wakuu wa wilaya na viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, asasi zisizo za
kiserikali, wadau wengine wa elimu, wazazi na walezi kuendelea kutoa
ushirikiano ili kuhakikisha uwepo wa miundombinu muhimu ya shule kwa ajili ya
wanafunzi wa elimu ya awali, msingi na sekondari,” alisema
Maoni ya kamati ya Bunge
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa, Jasson Rweikiza alishauri wakati akitoa maoni ya kamati hiyo kuwa
Serikali itoe fedha za miradi ya maendeleo kwa wakati
Alisema kufanya hivyo kutaziwezesha halmashauri kulipa
madeni ya wazabuni na wakandarasi kwa wakati na hivyo kuepusha ongezeko la
madeni katika miradi inayotelekeza
Mikoa iandae vipaumbele vichache kulingana na uwezo wa
bajeti na kusimamia kikamilifu utekelezaji wake, badala ya kuwa na msururu wa
vipaumbele ambavyo havitekelezeki kutokana na ufinyu wa bajeti,” alisema
Rweikiza.
Mishahara yafyeka bajeti ya Tamisemi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment