Wakati Rais John Magufuli akimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akague kwa kina sekta ya
madini, wabunge wamepokea kwa furaha mpango wa kuunda kamati ya Bunge
kuchunguza biashara ya madini nchini
Rais Magufuli aliagiza ukaguzi wa kina wa sekta hiyo jana
baada ya kukabidhiwa ripoti ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka jana na
mkaguzi huyo
Haiwezekani Watanzania wanakosa dawa hospitali wakati
dhahabu zao zinaondoka. Watanzania wanakosa maji wakati dhahabu zao zinaondoka.
Watanzania wanakosa umeme wakati dhahabu zao zinaondoka. Watanzania wanakosa
barabara wakati dhahabu zao zinaondoka,” alisema Rais akinukuliwa na taarifa
iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Rais.
Nataka ukakague kwa kina hii sekta ya madini ili Watanzania
wajue chao nini na kama kinapatikana sawasawa
Rais aliagiza ukaguzi ulenge kubaini mianya yote
inayosababisha nchi kukosa mapato makubwa, hususan katika misamaha ya kodi,
mikataba na ulipaji wa kodi.
Agizo hilo la Rais limekuja ikiwa ni siku moja baada ya
Spika wa Bunge, Job Ndugai kuahidi kuunda kamati kwa ajili ya kuchunguza
wanufaika wa biashara hiyo pamoja na mikataba yote ya madini
Pia ni siku moja tu baada ya Rais kutengua uteuzi wa katibu
mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Profesa Justin Ntalikwa aliyeongozana na
Spika Ndugai wakati alipotembelea bandarini juzi
Tanzania ni nchi ya nne kwa uchimbaji madini Afrika ikiwa
nyuma ya Afrika Kusini, Mali na Ghana. Sekta ya madini ilikuwa ikiendeshwa na
Serikali pekee hadi miaka themanini iliporuhusu wachimbaji wadogo. Katika miaka
ya tisini, sheria zililegezwa zaidi kuvutia kampuni ambazo zingeweza kuuza nje
bidhaa zitokanazo na madini na pia uwekezaji wa kampuni kubwa za nje ambazo
zilianza uchimbaji mkubwa
Mabadiliko hayo makubwa yanaonekana katika Sera ya Madini ya
mwaka 1997, Sheria ya Madini ya mwaka 1998 na ya mwaka 2010, ambayo iliongeza
mrabaha na kulazimisha kampuni za uchimbaji kusajiliwa katika Soko la Hisa na
kuipa Serikali umiliki katika miradi yote mipya ya uchimbaji madini
Wabunge wapongeza kamati Wakizungumzia uamuzi wa Spika
Ndugai kuunda kamati, wabunge waliohojiwa na Mwananchi walisema hiyo ni fursa
ya kulijadili kwa kina na kupata ukweli kuhusu mchanga huo wa madini
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John
Heche alisema ingawa usafirishaji wa mchanga umelisababishia taifa hasara, siku
zote makontena yamesafirishwa kihalali na kwa mujibu wa sheria na mikataba
ambayo taifa limesaini
Alisema kulisahihisha hilo hayahitajiki matamko, bali
kukusanya taarifa za kamati mbalimbali zilizowahi kuundwa kama ya Jaji Mark
Bomani ambayo ilituma mtu hadi Japan kufuatilia suala hilo, ili zijadiliwe
bungeni
Sheria zililetwa na kupitishwa kwa hati ya dharura, kuzuia
kwa ghafla tu vitu vilivyo kwenye mikataba ni kusababishia nchi hasara kubwa
zaidi.
Tayari Acacia wametangaza kwamba wanapata hasara ya dola
milioni moja za Kimarekani kwa siku baada ya mchanga wao kuzuiwa,” alisema
Heche. “Serikali ilete hiyo mikataba na sheria hizo zilizopitishwa kipindi
hicho bungeni tuzifanyie marekebisho. Kuendelea kutoa matamko tu kutasababisha
hasara kubwa kwa nchi,” alisema
Naibu katibu mkuu wa CUF-Bara, Magdalena Sakaya alisema
kuundwa kwa kamati hiyo kutaleta unafuu na ufumbuzi wa suala hilo kwa sababu
matokeo yataletwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa
Alisema ingekuwa kamati ya Serikali, wangekuwa na wasiwasi
lakini kwa kuwa ni ya Bunge wanaamini ripoti yake itawasilishwa kwenye chombo
hicho cha kisheria.
Sakaya, ambaye alisema amekuwa akihoji suala hilo tangu
mwaka 2011, alisema kamati za serikali zina tabia ya kuyeyuka kama ilivyokuwa
ya Operesheni Tokomeza
Wakati huo Waziri alikuwa William Ngeleja, lakini sikupata
jibu la msingi zaidi ya kuambiwa Taifa halina kazi nao kwa sababu hakuna
teknolojia ya kuchenjua makinikia hayo,” alisema
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, ambaye pia ni
mwenyekiti wa CCM wa mkoa, alisema ripoti ya kamati hiyo itaibua mjadala mpana
wa kulisemea suala hilo na kulipatia ufumbuzi
Alisema alianza kulilalamikia suala hilo tangu akiwa
mwenyekiti wa wilaya na baadaye mkoa , lakini hakuna aliyesikiliza.
>“Ninafahamu mengi kuhusu huo mchanga kwa sababu nipo
huko miaka mingi. Ninajua nini kinaendelea, lakini nisiende mbali zaidi
tusubiri kitakachobainishwa na kamati itakayoundwa,” alisema Msukuma
Akiunga mkono hoja ya suala hilo, mbunge wa Ukonga
(Chadema), Mwita Waitara alisema jambo la msingi ni kuangalia zaidi sheria ya
madini inasemaje
Hapa waziri wa sheria na wa madini wakutane wajadili kwa
kina kuhusu mikataba ya hao wasafirishaji na sheria zinasemaje kwa ujumla,”
alisema Waitara
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemshauri Rais
Magufuli kukutana na kuzungumza na wawekezaji wanaosafirisha mchanga wa madini
nje ya nchi ili kuweka mambo sawa na kuepusha hasara zaidi.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
imeonyesha wasiwasi wa Serikali kushitakiwa katika mahakama za kimataifa
kutokana na zuio hilo.
Akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo, mbunge wa
Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare alisema matarajio ni kwamba kampuni
za madini zitaipeleka nchi katika mahakama ya kimataifa. Hata hivyo, Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliwaondoa hofu na kuwataka kutulia
kwa sababu Serikali na mihimili mingine ya nchi, tayari imechukua hatua na
wataeleza matokeo baada ya uchunguzi kukamilika
Ripoti ya CAG Awali, Profesa Assad alimkabidhi Rais Magufuli
ripoti hiyo ambayo imegusa ukaguzi wa hali ya hesabu za Serikali, misamaha ya
kodi, ukusanyaji wa kodi na maduhuli ya Serikali, uandaaji na utekelezaji wa
bajeti, hali ya Deni la Taifa na usimamizi wa rasilimali watu
Mengine ni usimamizi wa mali na madeni ya Serikali na
usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma zikiwemo taasisi muhimu za kifedha
na Shirika la Umeme (Tanesco).
CAG alishauri Serikali kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza
kama mianya ya upotevu wa fedha za umma hasa katika madini
Mengine aliyoyaainisha ni kuiepusha Tanesco kununua umeme wa
gharama kubwa, matumizi mabaya ya misamaha ya kodi na kuongeza mashine za
kielektroniki za risiti (EFD).
Kadhalika, Rais alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kuitisha kikao cha pamoja kitakachomkutanisha CAG na mawaziri wote, makatibu
wakuu wa wizara zote, Gavana wa Benki Kuu na wakuu wa taasisi za umma ili kila
mmoja aambiwe hali ya hesabu ya taasisi yake na kuchukua hatua
Mheshimiwa Waziri Mkuu ukaongoze hicho kikao na wewe CAG
uwaambie kila mmoja katika eneo lake juu ya dosari zake, sitaki kuona dosari
zinajirudia zilezile kila wakati,” alisema Rais
Majaliwa azuia makontena 180
hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefanya ziara
Kahama mkoani Shinyanga jana jioni, alizuia makontena 180 yaliyokuwa
yamehifadhiwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi hadi hapo uchunguzi kuhusu
kiwango cha dhahabu kilichomo utakapokamilika
Majaliwa pia aliamuru kufunguliwa makontena zaidi ya matatu
na alichukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.
JPM amtaka CAG akague kwa kina madini, wabunge wafurahia kamati
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment