Polisi Yawazuia CUF Upande wa Maalim Kufanya Usafi Huku Abdul Kambaya na wenzake 6 Watiwa Mbaroni kwa Kuvamia Mkutano wa CUF
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa
CUF kufanya usafi katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni kutokana
na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana mvutano wa makundi
mawili.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika
mazingira ya ofisi za chama hicho, liliwasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah
Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.
Amesema kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa
muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama
wengine wanashauriwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake analoishi
au analofanyia kazi.
"Kitendo hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka
katika maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha
uvunjifu wa amani na atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za
kisheria," amesema Sirro.
Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu
waliovamia mkutano wa iongozi wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi
sasa wanawashikilia watu saba akiwemo Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama
hicho, Abdul Kambaya.
Amesema upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari
jalada limefikishwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi
ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Jeshi hilo pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari
yao kujitokeza katika Kituo cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na
kupatikana kwa magari matano yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.
Polisi Yawazuia CUF Upande wa Maalim Kufanya Usafi Huku Abdul Kambaya na wenzake 6 Watiwa Mbaroni kwa Kuvamia Mkutano wa CUF
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment