Mahakama ya hakimu mkazi arusha imetoa hukumu ndogo ya kesi
ya aliekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm arusha (UVCCM) Lengai Ole
Sabaya na kumuachi huru mshitakiwa baada ya jamuhuri kushindwa
kukamilisha ushahidi zaid wa kesi hiyo.
Akitoa hukumu hiyo ndogo hakimu mkazi Gwantwa Mwankuga
amesema kuwa awali kesi hiyo namba 376 ya mwaka 2016 ilifutwa na mahakama
ikashuhudia mshitakiwa huyo akikamatwa tena katika eneo la mahakama na
kufunguliwa kesi namba 493 mwaka jana.
Kufuatia tukio hilo mahakama inajiuliza ni kipi
kilichopelekea kukamatwa tena kwa mshitakiwa ambapo awali jamuhuri ilitakiwa
kuleta mashahidi wa kesi hiyo suala ambalo kwa upande wa muendesha mashitaka
hilo kuweza kufanikishwa ambapo jamuhuri imeeleza kuwa mashahidi wao wa muhimu
juu ya kesi hiyo mmoja yupo nchini kenya na mwengine yupo nje nchi.
Hakimu Gwantwa ameeleza kuwa baada ya kupitia shitaka hilo
na hoja za pande zote mahakama imekataa ombi ya mwendesha mashitaka hivyo
imeamua kumuachia huru chini ya kifungu namba cha sheria namba 225/5.
Lengai Ole Sabaya ambae pia ni diwani wa kata ya sambasha
wilayani arumeru alifikishwa mahakamani mwaka jana kwa tuhuma za kugushi
vitambulisho vya usalama wa taifa.
ALIEKUWA MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA AACHIWA HURU.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 28, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment