Wananchi
wanaishio katika mpaka wa Tanzania na Uganda Mutukula wameiomba tume ya
taifa ya uchaguzi kuwahakikishia kuwa uchaguzi unakuwa huru na wahaki
baada ya kuibuka vitendo vinavyo fanywa na baadhi ya wafuasi wa chama
tawala kutoa vitisho kwa wananchi kuchagua viongozi watokanao na hicho
pekee hali ambayo wamesema inaweza kuwanyima uhuru wao wa kikatiba wa
kuchagua kiongozi wamtakae.
Wakizungumza ITV kwa nyakati tofauti wakazi wa Mutukula wamesema
wamechoshwa na kero za mara kwa mara ikiwemo kupewa vitisho na wakati
mwingine kuitwa wahamiaji haramu kutokana na muingiliano mkubwa wa watu
kutoka nchi jirani ya uganda hali ambayo wamesema imepelekea hadi watu
wengine kuzuiwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga
nakwamba katika kipindihiki waliobahatika kujiandikisha wametunza
shahada zao kama mboni ya jicho huku wasikiliza kwa makini na
kuzichambua sera wagombea ili waweze kufanya maamuzi sahihi kwa
kumchagua kiongozi atakae tatua changamoto wanazokabiliana nazo
mipakani.
Hata wananchi hao hawakusita kulalamikia vizuizi vilivyoko katika
mpaka wa mtukula unaounganisha nchi za Tanzania na Uganda vimekuwa
kikwazo kikubwa kwa watanzania kushindwa kufanyabiashara katika mpaka
huu hali ambayo inawafanya wasinufaike na mzuguko wa biashara kutokana
na kodi kubwa wanazotozwa pindi wanaposafirisha biashara zao na kuongeza
kuwa kiongogozi atakae fanikiwa kuingia madarakani ahakikishe
anaimarisha uhusiano wa kibiashara kati yatanzania na nchi nyingine
jirani ili wananchi waze kuingia kwenye ushindani wa kibiashara katika
soko la afrika mashariki.
Mapema wakizungumza na wananchi katika kata ya Mutukula baadhi ya
viongozi wa chama cha ACT wazelendo wamewataka wananchi kupuuza vitisho
wanavyo vipata na kuchagua viongozi wa cha hicho kwanzia mgombea
ubunge wa jimbo la nkenge kwa tiketi ya ACT wazalendo evance kamenge na
mgombea urais wa chama cha ACT mama anna mghwira ndio watakao maliza
changamoto za kuondoa vizuizi Barabani na kuimarisha uhusiano wa
kibiasha kati ya tanzania na nchi nyingine barani Afrika.
CHANZO ITV
Wanachi waishio katika mpaka wa Tanzania na Mutukula wapewa vitisho.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 11, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment