Mgombea
urais kupitia chama cha chadema anayeungwa mkono na vyama vinne
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa Edward Lowasa ameahidi
kuboresha mishahara ya walimu na kulipa stahiki zao zote kama watanzania
watampa ridhaa kuwa rais wa nchi.
Akiwa mjini tarime Edward Lowasa alifanikiwa kuhutubia mikutano
katika maeneo yasalali,nyamongo na mgumu kabla ya kuhitimisha kwa
kuhutubia maelf ya wakazi wa mji wa tarime katika uwanja wa sabasaba
Baada ya kuhitimisha kwa kishindo kanda ya kaskazini sasa ni rasmi kanda ya ziwa akianzia tarime mkoani Mara.
Edward Lowasa anayetajwa kama mkombozi wa tanzania ijayo, amesema
ni dhamira yake kuona mtanzania akineemeka na keki ya taifa huku suala
la elimu kwake akisema ndio itakuwa slaha kubwa ya kuifikisha Tanzania
panapotakikana.
Fredric Sumaye waziri mkuu mstaaf amesema wanatarime na watanzania
kwa ujumla hawanabudi kuitumia vema Oct 25 kwa kukiondosha chama cha
CCM kwani kuna kila dalili ya kuchokwa na watanzania.
Lowassa aahidi kuboresha mishahara ya walimu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 11, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment