Kiongozi wa chama cha upinzani
nchini Mozambique Afonso Dhlakama aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani
siku ya ijumaa alipokuwa akirudi kutoka mafichoni baada ya shambulizi la
risasi lililowaua wanachama 23 wa ujumbe wake.
Wanachama wake wa usalama walikamatwa huku wakaazi wanaoishi katika eneo hilo wakiagizwa kuondoka huku idadi kubwa ya wanajeshi na maafisa wa polisi wakisalia nje ya nyumba hiyo.
Chama cha Renamokinachoongozwa na Dhlakama kilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 16 dhidi ya kile cha Frelimo ambavyo vilimalizika na makubaliano ya amani ya mwaka 1992.
Wasiwasi umezuka tena,katika kipindi cha miaka michache iliopita ,ikiwemo kipindi kilichokaribia uchaguzi wa Octoba mwaka jana ambao Renamo ilishindwa.
Serikali haijatoa sababu ya kukamatwa,ijapokuwa ilisema mwezi uliopita kwamba shambulio hilo la risasi lilianza baada ya maafisa wa usalama wa Dhlakama kuifyatulia risasi texi ya raia.
Lakini Chama cha Renamo kimekana hilo kikisema kuwa Msafara wa Dhlakama ulivamiwa.
''Kizuizi alichowekewa Afonso Dhlakama ni shambulio linalolenga demokrasia na sheria'',mbunge wa chama cha Renamo Ivone Soares alikiambia chombo cha habari cha Reuters.
''Serikali na Frelimo hawawaambii raia wa Mozambique ukweli kwa kuamua kutumia nguvu badala ya mazungumzo''.
Kiongozi wa upinzani azuiliwa nyumbani Moz
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 11, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment