Aliyemzushia kifo Mwamunyange mahakamani.


 Mwanafunzi aliyesambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange, amelishwa sumu, jana amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi huyo, Benedect Ngonyani (24), alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, Charles Mwaijage.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, alidai kuwa Septemba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alisambaza taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa facebook kwamba CDF, amelishwa sumu.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alisambaza taarifa hizo huku akijua siyo za kweli na kwamba zina lengo la kupotosha umma.
Mshtakiwa alikana shitaka hilo.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), amewasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi Ngonyani kwa maslahi ya taifa.

Hakimu Mwaijage alisema mshtakiwa apelekwe mahabusu hadi Oktoba 23, mwaka huu kesi yake itakapotajwa.

Wakati huo huo, raia watatu wa Pakstan, Hafeez Irfan (32), Mirza Baig (41) na Irfan Baig, wanakabiliwa na shitaka la kula njama ya kuingiza mitambo na kuingilia mawasiliano ya kimataifa na kuisababishia serikali na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya Sh. Milioni 140,049.
Chanzo: NIPASHE
Aliyemzushia kifo Mwamunyange mahakamani. Aliyemzushia kifo Mwamunyange mahakamani. Reviewed by KUSAGANEWS on October 11, 2015 Rating: 5

No comments: