Rais kikwete amefungua kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM.



Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM rais Jakaya Kikwete amefungua kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM ambapo amesema mchakato wa kutafuta majina matano ya wagombea urais ndo kwanza umeanza.

Kikao hicho kinajumuisha marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu pamoja na wajumbe ambapo mwenyekiti huyo mara baada ya kuwasili ukumbini amesema mchakato huo umeanza rasmi baada ya kikao cha maadili kumalizika huku katibu mkuu wa chama hicho Bw Abdulrahman Kinana akidai kuwa akidi ya wajumbe imetimia.
 
Akizungumzia mchakato huo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Bw Nape Nnauye amelalamikia taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais kuwa zinaathiri kwa kiasi kikubwa mchakato huo na kuongeza kuwa uchelewaji wa kumpata mgombea umesuasua kutokana na mwenyekiti wa chama hicho kukabiliwa na majukumu mengi ya kitaifa.
 
Baadhi ya wajumbe wa NEC waliopo mjini Dodoma wameeleza kuwa na matumaini kuwa chama chao kitateua mgombea anayekubalika na kuwataka watanzania wakiwepo mashabiki wa baadhi ya wagombea kuwa na subira.
 
Hata hivyo katika eneo la makao makuu ya CCM kumekuwa na hekaheka za wajumbe lakini na wananchi mbalimbali ambao wanasubiri kwa hamu kubwa majina matano yatakayoteuliwa ndani ya kikao hicho huku ulinzi ukiwa umeimarishwa ambapo ITV imeshuhudia polisi pamoja na farasi zikiwa zinafanya doria katika maeneo hayo
Rais kikwete amefungua kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM. Rais kikwete amefungua kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM. Reviewed by KUSAGANEWS on July 10, 2015 Rating: 5

No comments: