JESHI
la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni linawashikilia watu watano kwa tuhuma za
kuchoma kituo kidogo cha Polisi kilichopo Bunju ‘A’ jijini Dar es Salam.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Camillus Wambura alisema tukio hilo lilitokea saa
3:00 asubuhi wakati Tanroads pamoja na Jeshi la Polisi walipokuwa katika
mazungumzo ya kuweka matuta katika barabara hiyo.
Alisema
kabla ya kuchomwa kituo hicho dereva aliyetambulika kwa jina la Yohana John
aliyekuwa akiendesha gari aina ya Coaster alisababisha ajali katika eneo hilo
na kumgonga mwanafunzi mmoja
wa shule ya Bunjua ‘A’ Radhia
Omary na kusababisha kifo chake.
Alisema
baada ya mwanafunzi huyo kupoteza maisha wanafunzi wa shule hiyo pamoja na
wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kulala barabarani hali iliyosababaisha magari
kutoendelea na safari zake.
Alisema
wananchi hao pamoja na wanafunzi walifunga barabara hiyo kwa muda wa saa tatu
wakidai kuwa wanataka matuta yawekwe katika eneo hilo lililopo karibu na shule
hiyo ili liweze kuwasaidia wanafunzi wakati wa kuvuka barabara.
Hali
hiyo ilileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa kufungwa na kushindwa
kuendelea na shughuli zao hali iliyosababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya
watu.
“Baada
ya tukio hilo polisi na Tanroads tulikaa kikao cha dharura kilichokuwa
kikielekeza utengenezwaji wa matuta ya haraka katika eneo hilo.
“Wakati
tukiendelea na mazungumzo hayo wananchi walipata mwanya wa kukivamia kituo
hicho na kukichoma moto.
“Sababu
ya wananchi hao kuchoma
kituo hicho hakuna, na wamefanya jambo ambalo si la busara na wamesahau kuwa
kituo hicho kinawasaidia watu wote wa eneo hilo,” alisema Kamanda Wambura.
Alisema
mbali na kuchoma kituo hicho pia wamechoma magari mamne ya watu binafsi
yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa
kituo hicho.
Pia
alisema wanamshikilia dereva wa Coaster aliyesababisha ajali pamoja na gari hilo.
“Kwa
sasa tupo katika zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu wote
waliosababisha vurugu hizo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,” alisema
Kamanda Wambura.
Shuhuda
wa tukio hilo, Moshi Sultan, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 3:00 asubuhi
baada ya gari kumgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa anakwenda shule.
Alisema
baada ya tukio hilo wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kufunga barabara
hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuanza mvutano kati yao na hatimaye
wananchi hao kuvamia kituo hicho na
kukichoma moto.
Alisema
wananchi hao waliwasha moto kituoni hapo pamoja na tairi za gari na kudai kuwa askari waliopo hawafanyi kazi
kwa umakini.
“Kutokuwapo kwa askari wa kutosha katika kituo hicho
kumechangia wananchi hao kuvamia kwa urahisi na kuchoma moto kituo
hicho,”alisema.
Katika
tukio jingine, moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba yote inayomilikiwa na
Hamisi Katori iliyopo katika mtaa wa Mabanda Marefu Ukonga Mombasa jijini Dar
es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Lucas Mkondya, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Alisema
wakati moto huo ukiendelea kuwaka alikuwepo mtoto mdogo mwenye umri wa miaka
miwili aliyetambulika kwa jina la Mohamed Shabani ambaye alikuwa amelala ndani
lakini msamaria mwema alifanikiwa kumuokoa.
Mkondya
alisema moto huo uliteketeza nyumba yote, mali na thamani zilizoteketea kwa
moto bado hazijafahamika.
Alisema
hakuna madhara kwa binadamu, moto ulizimwa na kikosi cha Zimamoto Uokoaji cha
Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.
Polisi
wa wakijaribu kuwatawanya watu katika eneo la kituo cha Polisi Bunju
baada ya wanachi kukichoma moto baada ya mwanafunzi wa shule kugongwa na
gari na kufa papo hapo.
No comments:
Post a Comment