Bingwa wa rekodi ya dunia katika
mbio za mita 800 Dunia mkenya David Rudisha ameshindwa tena kwa mara
nyengine katika mbio hizo na Bingwa katika mbio hizo Nijel Amos wa
Botswana.
Rudisha tayari alikuwa ameongoza mbio hizo akiwa mbele
na ilikuwa imesalia mita 300 kufika katika utepe,wakati Nijel Amos
alipotoka nyuma na kumshinda.Rudishawakati huohuo mwanariadha wa Marekani Justin Gatlin aliweka mda bora wa pili mwaka 2015 baada ya kumshinda Asafa Powel na Tyson Gay katika mbio za mita 100 katika mbio za Diamond League mjini Lausanne
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye amehudumia mara mbili marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda wa sekunde 9.75 kabla ya mashindano ya mwezi ujao ya dunia.
Powell na Gay wote wamekimbia mda wa sekunde 9.92 huku Usain Bolt akiwa bado anauguza jeraha,ijapokuwa ana mpango wa kutetea taji lake katika mbio za Olimpiki mjini Beijing.
Nijel Amos amshinda tena Rudisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 10, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment