DAWA ya jeuri kiburi. Usimuulize Cristiano Ronaldo swali analoliona la kijinga, ataondoka zake. Ndicho kilichotokea juzi Jumapili baada ya kuulizwa kama Sergio Ramos ataondoka Santiago Bernabeu au hataondoka.
Ramos amekerwa na hali ya mkataba wake Santiago
Bernabeu na inadaiwa kuwa ameipa timu hiyo mpaka Ijumaa wiki hii kutatua
suala la mkataba huo kabla ya Real haijatimkia katika ziara yake katika
nchi za Australia na China.
Inadaiwa kuwa wiki iliyopita United ilitoswa
katika dau lake la Pauni 35 milioni na Real Madrid kwa ajili ya staa
huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye anaamini kuwa Madrid imeweka pesa
kiduchu katika mkataba wao mpya.
“Sijui. Sijui,” Alisema Ronaldo huku akionekana
kukasirishwa na swali hilo na kuamua kuvua vipaza sauti na kuondoka
studio. Lakini kabla hajaondoka, Ronaldo alikiri kwamba hana matatizo
na kocha mpya wa klabu hiyo, Rafa Benitez na kudai kwamba atafanya naye
kazi vizuri.
“Sijawahi kufanya kazi na yeye, lakini ni kocha
mwenye uzoefu mkubwa. Tuone kitakachotokea. Real Madrid ni klabu kubwa
duniani. Siku zote inatoa changamoto kwa wachezaji na makocha,” alisema
staa huyo wa kimataifa wa Ureno.
“Ningependa kufanya kazi na yeye. Tuone kama tunaweza kushinda mataji muhimu. Nina uhakika na hilo.”
Hata hivyo, ni uhamisho wa Ramos ndiyo ambao
unaonekana kuzua kizaazaa nchini Hispania na barani Ulaya kwa jumla.
Juzi, staa wa Barcelona, Andres Iniesta ambaye timu yake ina upinzani wa
kufa na Real Madrid alikiri kwamba haoni kama mchezaji huyo anaweza
kuruhusiwa kuondoka.
“Siku zote nimesema kuwa Sergio ni mmoja kati ya
mabeki bora wa kati duniani. Tayari yupo katika timu kubwa, lakini
kusema kweli sioni Madrid wakimruhusu kuondoka,” alisema Iniesta.
Mmoja kati ya wachambuzi mahiri wa soka la
Hispania, Graham Hunter, alidai kwamba anadhani dili la mchezaji huyo
kwenda Manchester United litafanikiwa kwa sababu mwenyewe ameomba
kuhama.
“Ramos ameimbia Madrid moja kwa moja kwamba
anataka kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto. Amewataka
waanze mazungumzo na Manchester United na hataki Real iongee na timu
yoyote zaidi ya Manchester United,” alisema Hunter.
Hata hivyo, beki wa zamani wa Manchester United,
Rio Ferdinand ambaye ameachana na soka, amedai kwamba haoni kama Ramos
atakwenda Old Trafford
KIBURI SANA: Ronaldo akasirishwa na swali la Ramos, aondoka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 10, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment