Shambulio limetokea kaskazini mashariki mwa Kenya
ambapo inahofiwa kuwa takriban watu 11 wameuawa. Shambulio hilo linaaminiwa
kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokua wenyeji.
Walioshuhudia
wameambia BBC kuwa walisikia mwanzo milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio
ya risasi. Shirika la msalaba mwekundu linaongoza oparesheni ya kuwaokoa
majeruhi ambao idadi kamili haijulikani bado.
Nani washambuliaji ?
Haijathibitishwa
pia ni nani waliofanya shambulio hilo japo wanamgambo wa Al shabaab wamekuwa
wakilenga wakaazi wasio wenyeji wa asili katika eneo hilo katika mashambulio
yaliyotangulia.
Shambulio
kama hilo dhidi ya wachimba migodi lilitokea jijini Mandera mwezi Disemba 2014,
ambapo takriban watu 36 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Marudio ya shambulio
Mashambulio
kama haya yametishia kudumaza shughuli katika eneo la kaskazini mashariki mwa
Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake ni watu kutoka maeneo mingine ya Kenya.
Wafanyikazi
hawa wamekuwa wakidai kutishiwa maisha, na wengi wa wafanyikazi kama vile
walimu na hata wahudumu wa afya wamesusia kurejea kazini katika eneo hilo
wakidai kutishiwa maisha yao.
Chini
ya siku kumi zilizopita serikali ya Kenya iliondoa marufuku ya kutoka nje
kuanzia magharibi hadi alfajiri, kufuatia wito kutoka kwa viongozi wa kiislamu
waliodai kuwa marufuku hiyo inahujumu ibada za waislamu za usiku katika mwezi
wa Ramadhani.
Asili
mia kubwa ya wakaazi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya, ni waislamu
wa asili ya kisomali.
11 wauawa katika shambulio Mandera,Kenya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 06, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment