Matukio ya utekaji wanahabari, kuibuka kundi la watu
wasiojulikana, kufungiwa vyombo vya habari na kupigwa faini kwa vyombo hivyo
vimetajwa kudunisha uhuru wa habari nchini
Wakisoma hotuba zao leo Mei 3 katika maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Vyombo vya
habari kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania, (Misa- Tan) Salome Kitomari
amesema ni muhimu hatua zichukuliwe kukabiliana na hali iliyopo sasa
Kitomari amesema, takwimu za taasisi kama waandishi
wasio na mipaka na kamati ya kulinda waandishi wa habari zinaonesha
kushuka viwango vya uhuru wa habari na kujieleza Tanzania
"Lakini pia matukio ya utekwaji nyara na viwango vya
unyanyasaji wa wanahabari duniani vimeongezeka sana"amesema
Amesema mwaka jana zimeripotiwa kesi za kupotea kwa
waandishi wa habari, manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari
“Leo ni siku ya 163 tangu kupotea kwa mwandishi wa habari wa
Mwananchi, hakuna hata fununu tu yupo wapi ama yupo hao ni jambo ambalo linatia
doa nchi yetu,"amesema
Amesema wahabari wanaitaka Serikali kupitia jeshi la polisi
kuwatafuta waliohusika na kitendo hicho na kuwachukulia hatua za kisheria
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, (TEF)
Deodatus Balile amesema mazingira ya kazi ya kuandika habari yamekuwa
magumu kutokana na baadhi ya watendaji wa vyombo vya dola kubugudhi na
kuwafanyia uonevu wanahabari, huku kukiibuka kundi la watu wasiojulikana
Kiwango cha unyanyasaji wa wanahabari duniani chaongezeka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment