Balozi wa Ethiopia Nchini Tanzania amefanya mahojiano na
Alloyce Nyanda kuhusu mzozo unaondelea
huko nchini Ethiopia ( Northern Part of
Ethiopia) na kutoa msimamo wa serikali ya Ethiopia juu ya swala hilo
Katika mahojiani hayo
yaliyofanyika jijini Dar Es salaam Mhe. Balozi Shibru Mamo Kedida amesema kuwa serikali ya Ethiopia inazingatia zaidi haki na Uhuru wa watu wa
Ethiopia katika kupata Maendeleo.
“Maendeleo ni haki ya kila Mwanachi na ni swala la kuonyesha
ni jinsi gani Maendeo ndio msingi mkubwa wa ustawi wa watu wetu “ amesema
Balozi Mamo
Aidha mahojiano hayo
yamempa fursa Balozi kutoa msimami na mtazamo juu ya ujenzi
wa Bwala kubwa la umeme linalojengwa nchini Ethiopia ambalo litaleta
Mapinduzi makubwa ya uchumi,ajira kwa Wananchi wa Ethiopia na afrika kwa
ijumla kwa kuwa ujenzi huo hauna madhara
yoyote kwa afrika zaidi ya Faida.
Ifahamike kuwa Ethiopia imekuwa ikipata shtuma kutoka
nchini Misri kwa kutumia mto Nile kujenga bwawa la Umeme ambalo misri wanadai hawana haki ya kisheria
kutumia Mto Nile
Mahojiano zaidi usikose kufuatilia Kipindi cha The Big
Ajenda na Mtozi Alloyce Nyanda kupitia star Tv
No comments:
Post a Comment