Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya
uhujumu uchumi namba ya mwaka 2022 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa
Jiji la Arusha Dakta John Pima na wenzake wawili wameuomba upande wa mashtaka
kuharakisha upelelezi ili washtakiwa waweze kupata haki zao.
Mbali na Dakta Pima wengine katika shauri hilo
ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya mipango na uchumi,Innocent Maduhu na aliyekuwa
Mkuu wa idara ya fedha katika halamshauri hiyo,Mariam Mshana.
Shauri hilo ambalo lilipangwa leo kwa ajili ya
kutajwa ambapo wakili wa Jamhuri Upendo Shemkole aliiambia mahakama kuwa
upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa
ajili ya kutajwa .
Wakili wa utetezi Sabato Ngogo aliiomba upande
mashtaka kuharakisha upelelezi huo ili washtakiwa waweze kupata haki yao na
kama upelelezi unawasumbua waliondoe shitaka.
Katika kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba 3
inayomkabili Dakta Pima na wenzake watatu ambao ni Mshana,Maduhu na Nuru Ginana
aliyekuwa mchumi wa jiji hilo,washitakiwa hao walishindwa kusomewa maelezo ya
awali katika kesi hiyo.
Wakili Upendo aliieleza mahakama kuwa shauri
lilipangwa kwa ajili ya kuwasomea mwashitakiwa hao amelezo ya awali ila
wanaomba kupangiwa tarehe nyingine bila kutoa sababu yoyote.
Baada ya maelezo hayo,Wakili Sabato aliieleza
mahakama kuwa leo ni mara ya tatu maelezo hayo kushindwa kusomwa huku kukiwa
hakujatajwa sababu yoyote wakati walishasema upelelezi umekamilika.
Wakili huyo aliomba mahakama iangalie
mshitakiwa wa pili(Mariam) ana mtoto mdogo na kuwa watuhumiwa hao wanateseka na
kuomba mahakama itoe amri kuwa tarehe itakayopangwa maelezo hayo yaweze
kusomwa.
Wakili wa jamhuri alisema amesikia hoja
na hakusema awali kwa kuwa maelezo hayo hayapo tayari na katika tarehe
inayotajwa watafanyia kazi ili kesi iweze kuendelea.
Katika kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba
4/2022 inayomkabili Dakta Pima,Mariam,Madumu na Alex Daniel,ambayo pia
ilipangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali,ilishindwa kuendelea baada ya
jamhuri kueleza kuwa maelezo hayo hayapo tayari.
Wakili Sabato aliomba washitakiwa hao wasomewe
mapema maelezo hayo ili haki iweze kutendeka kwa washitakiwa hao.
Hakimu Mbelwa aliahirisha kesi zote tatu
hadi Agosti 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment