Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Kiseri Ndaletyan (38) mkazi wa kitongoji cha Naamalasin kata ya Noondoto tarafa ya Kitumbeini Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha amefariki dunia baada ya kukatwa kitu chenye ncha kali shingoni na mdogo wake Melita Ndaletyan (34).
Kwa mujibu wa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia leo Julai 8,2021 majira ya saa sita na nusu katika kitongoji cha
Naamalasin kata ya Noondoto tarafa ya Kitumbeini Wilaya ya Longido.
Chanzo cha tukio hilo
ni tamaa ya kimapenzi, baada ya mtuhumiwa Melita Ndayetyan kutaka kumuingilia
kimwili mke wa kaka yake na kuzuiwa na marehemu kufanya jambo hilo",amesema Kamanda Masejo.
Amesema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika jarada litapelekwa Ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Kamanda Masejo pia ametoa ufafanuzi kuhusu tukio la ukatili dhidi ya mtoto mdogo mwenye umri miaka minne(04) ambaye jina lake limehifadhiwa Mkazi wa Majengo jijini Arusha aliyekutwa ametelekezwa maeneo ya Burka kata ya Olasiti Tarafa ya Elerai katika jiji la Arusha.
"Tarehe 06/07/2021 muda wa 12:00hrs huko maeneo ya Burka kata ya Olasiti Tarafa ya Elerai katika jiji la Arusha,Mtoto mdogo umri miaka minne (04) jina lake limehifadhiwa Mkazi wa Majengo jijini Arusha, alikutwa ametelekezwa maeneo ya Burka.
"Taarifa za awali
zilibaini kwamba mtoto huyo alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa
majani mdomoni na baba yake wa kufikia. Jeshi la Polisi liliendelea na
upelelezi na kubaini kwamba, kuna mgogoro wa kifamilia kati ya mama wa mtoto
huyo na baba wa kufikia jina limehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi",ameeleza.
"Nitoe wito kwa
wananchi kutoa taarifa dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa watoto kwa Jeshi la
Polisi ili kukomesha au kumaliza kabisa tatizo la unyanyasaji kwa watoto. Pia
niwaonye wenza wenye migogoro katika familia kufikisha matatizo yao katika
mamlaka husika na sio kujichukulia hatua za kuhamishia hasira zao kwa watoto na
wenza wao",ameongeza.
No comments:
Post a Comment