RC MGHWIRA AAGIZA MKUU WA KITUO KUCHUKULIWA HATUA MARA MOJA

 

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza mkuu wa kituo cha polisi Holili Wilaya ya Rombo pamoja na askari wawili kuchukuliwa hatua kwa madai ya kuzembea na kuruhusu pikipiki kutoka Kenya na Tanzania kusafirisha mahindi kwa magendo.

Amechukua uamuzi huo leo Ijumaa Aprili 2, 2021 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mpaka wa Holili wilayani Rombo na kushuhudia shehena ya mahindi yakiwa yamepakiwa kwa ajili ya kusafirishwa nchini Kenya.

Mahindi hayo yamekuwa yakisafirishwa kwa magendo baada ya Kenya kuweka katazo la mahindi kutoka Tanzania kuingia nchini humo kwa madai ya kuwa yana sumu kuvu.

"Jana nilikuja hapa mchana nikauliza kama kuna kitu kinaendelea hapa Holili wakaniambia hakuna kitu baada ya mizigo yetu yote kurudi Tanzania. Nilipoambiwa hivyo sikuridhika nilirudi ofisini nikafanya kazi zangu lakini baadaye nikawaambia watu wangu watangulie wakaone hali ilivyo. Walipofika wakaniambia vijana wa bodaboda wanafanya kazi kama mchwa ya kusafirisha mahindi kwa kutumia njia za panya kupeleka Kenya.”

“Cha kushangaza askari anafika kwenye lile eneo na kuwaambia wale bodaboda waondoke. Kama askari wetu ndio mnatugeuka na kufukuza watu kwa kuwaambia ondokeni na watu hao wanatuvunjia sheria, kupoteza mapato na kutuharibia biashara..., kwa utaratibu huu naomba askari hawa pamoja na mkuu wa kituo hiki wachukuliwe hatua za kinidhamu," amesema Mghwira

RC MGHWIRA AAGIZA MKUU WA KITUO KUCHUKULIWA HATUA MARA MOJA RC MGHWIRA AAGIZA MKUU WA KITUO KUCHUKULIWA HATUA MARA MOJA Reviewed by KUSAGANEWS on April 02, 2021 Rating: 5

No comments: