Ndani ya saa 48, askari watatu wa Jeshi la Polisi wamejiua
kwa kujipiga risasi, mmoja akiacha waraka ukihusisha wivu wa kimapenzi
Konstebo Nelson William (28), alijiua juzi saa tisa alasiri
kwa kujipiga risasi iliyofumua kichwa katika kituo kidogo cha Polisi Natta
wilayani Serengeti mkoani Mara kwa sababu ya wivu wa mapenzi na mwili
ulisafirishwa jana kwenda Iringa kwa mazishi na askari wengine wawili walijiua
mmoja Tabora na mwingine Morogoro
Taarifa ya polisi inasema Jumanne saa 12 asubuhi askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Tabora, Michael Hosea alijiua kwa
kujipiga risasi nne kichwani muda mfupi kabla ya kuelekea lindoni. Jana, pia
saa 12 asubuhi, mkufunzi katika chuo cha maofisa wa polisi Kidatu wilayani
Kilombero, Benedict Nyamagatara alijiua kwa risasi
Tukio la Morogoro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa
alisema Nyamagatara aliyekuwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi alijipiga risasi
kwenye taya na kutokea kichwani.
Alisema ofisa huyo alikuwa zamu akiwakagua askari wengine na
kutoa maelekezo ya kazi ndani ya chuo. Alisema alitumia silaha ya mmoja wa
askari kujipiga risasi.</p></div><div><p>Kamanda
Mutafungwa alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kiwanda
cha Sukari Kilombero One (K1) na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea
Tabora
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tabora, Graifton Mushi alisema askari wa FFU Hosea alijiua kwa
kujipiga risasi nne baada ya kuiweka bunduki aina ya SMG shingoni.</p></div><div><p>Alisema
awali, askari huyo alichukua bunduki katika ghala kuelekea lindoni Benki ya
Access mjini Tabora umbali wa kilomita moja na nusu kutoka kituo cha FFU
Kamanda huyo alisema chanzo cha kujiua askari huyo
hakijajulikana na uchunguzi unaendelea akibainisha mara nyingi matukio ya aina
hiyo hutokana na msongo wa mawazo.
Alisema ni vizuri
watu wanapokuwa na tatizo waeleze ili kupatiwa ushauri au kusaidiwa kuliko
kukaa kimya na hatimaye kuchukua uamuzi wa kujiua
Askari aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini
alisema Hosea alionekuwa kuwa mtu mwenye mawazo mengi katika siku za hivi
karibuni
Waraka haujasomwa
Katika tukio la Serengeti, inadaiwa kuwa konstebo William
(28) aliacha waraka akitaka usomwe wakati mwili wake ukiagwa akieleza kuwa
sababu ya kujiua ni mgogoro kati yake na mpenzi wake. Hata hivyo, ujumbe huo
haukusomwa jana
Mwanamke aliyetajwa katika waraka huo (jina linahifadhiwa)
hakufika kuaga mwili ikielezwa na ndugu zake kuwa hali yake kiafya si nzuri.
Mwili wa askari huyo uliagwa katika hospitali teule ya Wilaya ya Mugumu
Baadhi ya askari wakizungumza kwa sharti la majina yao
kutotajwa walidai kuwa mwenzao hakufurahishwa na uamuzi wa viongozi wao
kumlazimisha kulipa vyombo alivyovunja wakati wa ugomvi na mpenzi wake kwa kuwa
vilikuwa mali yake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alisema hakuna
anayeshikiliwa kuhusiana na tukio la kujiua kwa askari huyo na kwamba
wanaendelea kufuatilia waraka unaodaiwa kuwa aliuandika
Imeandikwa na Anthony Mayunga (Serengeti), Robert Kakwesi
(Tabora) na Lilian Lucas (Morogoro).
Polisi watatu wajiua kwa risasi ndani ya saa 48
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment