Spika wa Bunge la Tanzania
mheshimiwa Job Ndugai amewataka vijana nchini kugombea nafasi mbalimabali
za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge ili kutatua tatizo la kukosa ajira
kutokana na kukosa uzoefu.
Spika Ndugai amesema hayo Bungeni
leo, Mei 18, 2018 baada majibu ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na
Bunge, Jenista Mhagama, kutokana na swali la mbunge wa viti maalumu Zainab
Katimba aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa
vijana wasomi wasikuwa na uzoefu.
“Asante sana Waziri wa nchi kwa
majibu ya nyongeza, Vijana wasomi, zipo kazi nyingine hazihitaji uzoefu,
mnaweza mkagombea Udiwani, mkagombea Ubunge, nawatangazia vita waheshimiwa
hapa” amesema Spika Ndugai.
Awali Naibu Waziri, Sera, Bunge,
kazi, vijana, ajira na walemavu Anthony Mavunde amesema kwamba serikali
imeendaa utaratibu wa kuwapa vijana nafasi za kujitolea katika makampuni na
mashirika mbalimbali ili kupata uzoefu wa kuweza kuajiliwa
“Kupitia mpango huu utawasaidia sana
vijana wasomi wa nchi yetu ambao walikuwa wakipata tabu na kikwazo cha
uzoefu, kwa hivi sasa atapata nafasi ya kujifunza katika kampuni kwa muda huo
wa mwaka mmoja na badae tutampatia cheti cha kumtambua ili iwe kama
kiambatanisho chake” amesema Naibu Waziri Mavunde.
Vijana mgombee Udiwani na Ubunge - Ndugai
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment