Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye
ameitaka Serikali kutoona aibu kuiondoa bungeni bajeti ya Wizara ya Kilimo
mwaka 2018/19 ili ikajipange upya kwa maelezo kuwa bajeti hiyo itaiumiza
Serikali ya Awamu ya Tano
Nape pia amehoji zilipo fedha ambazo
Serikali imekuwa ikijigamba kuwa imekusanya kwa kiasi kikubwa wakati hakuna
fedha katika miradi ya maendeleo
Nape ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 16,
2018 wakati akizungumza katika mjadala wa bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma
Waziri huyo wa zamani wa habari amesema
umefika wakati wa kueleza ukweli kuwa bajeti ya wizara hiyo ni ngumu na
haiendani kabisa la Ilani ya uchaguzi ya CCM, ikipitishwa itakuwa mwiba kwa
Serikali
Amesema anamuonea huruma Waziri wa Kilimo,
Dk Charles Tizeba kwa maelezo kuwa kuna mambo yaliyo nje ya uwezo wake,
lakini kila jambo anabebeshwa yeye
“Ni mtihani mkubwa kwa Serikali katika
bajeti ambayo inagusa asimilia 80 ya Watanzania. Bajeti hii inagusa maisha ya
watu hivyo ujumbe unaotakiwa kwa wananchi ni je, Serikali inajali maendeleo ya
vitu au watu waliowaweka madarakani jambo ambalo majibu yake yatakuwa na maana
tofauti kwa wananchi.”
Amesema Serikali haiwajali wakulima
kwa maelezo kuwa imekuwa ikipunguza bajeti hiyo kuanzia mwaka 2018/17
“Wakati fulani tulisema Serikali ikwepe
kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi mikubwa inayoweza kujiendesha kibiashara,
lakini tukashambuliwa kama si wazalendo katika nchi hii, na hili Tizeba
tutakubebesha bure lakini si lako,” amesema Nape
Amesema akikubali bajeti hiyo, wananchi wake
wa Mtama na wakulima wa korosho, ufuta, pamba na mazao mengine nchini
watamshangaa kwa kiasi kikubwa hivyo hakuna shida wala aibu kukaa pamoja na
kuifumua kama ilivyowahi kufanyika kwa wizara nyingine
Alisema Ilani ya uchaguzi wa CCM ilitamka
kuwa Serikali itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuwasaidia wakulima kutafuta
masoko ya nje lakini kwa sasa imekuwa kinyume kabisa na ilani hiyo, kwamba
kukaa mezani ndio suluhu
“Ukimwambia mtu akale magunia 20 ya mbaazi
si unamtukana huyu, hivi tunawaambia nini wakulima katika jambo hili, ni kwa
nini tusiwe wepesi wa kukubali ushauri na kuzungumza kwa pamoja,” amehoji
Nape ataka bajeti Wizara ya Kilimo kuondolewa bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment