Waandishi wa habari kutoka katika
redio tano za mikoa minne nchini inayoongoza kwa ukeketaji,watendaji wa
vijiji,viongozi wa kimila,viongozi wa dini,Mganga wa jadi na maafisa
ustawi wa jamii wamekutana katika warsha ya siku tatu halmashauri ya wilaya
Ngorongoro Mkoani Arusha kujadili kuhusu kampeni ya kupambana na ukeketaji na
ndoa za utotoni.
Mikoa iliyopo katika kampeni hiyo ni
Arusha, Manyara, Dodoma na Mara.
Katika wilaya ya Ngorongoro taarifa
za ukeketaji zinasikitisha kwa namna takwimu za awali zinavyoeleza kwani kwa
miaka mitatu tangu 2016 hadi 2018 ukeketaji unaongezeka badala ya
kupungua.
Mratibu wa huduma za Afya kwa Mama
na mtoto wilayani Ngorongoro Anna Masago amesema Kati ya wanawake 2991
waliofika hospitalini kwaajili ya huduma ya afya wakinamama 1783 ambayo ni
asilimia 66% wamegundulika kuwa wamekeketwa
Mwaka 2017 wanawake 2731 walioenda
hospitalini Kati yao 2201 waligundulika kukeketwa ambao sawa na asilimia 81% na
mwaka 2018 mwezi January hadi mach wanawake 869 Kati yao 751 sawa na asilimia
86% wamegundulika kukeketwa.
Kufuatia ripoti hiyo Mkurugenzi wa
halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Siumbu amesikitishwa na takwimu
hizo huku akieleza kuwa halmashauri yake ndiyo iko nyuma katika masuala ya
maendeleo huku akielezwa kuwa sababu inayopeleka Hali hiyo ni wakazi wa eneo
hilo kushikilia mila potofu.
Kupitia warsha hiyo iliyoandaliwa na
shirika la umoja wa Kimataifa la Elimu, sayansi, na utamaduni-UNESCO,Mkurugenzi
wa halmashauri ya hiyo ameomba elimu zaidi ielekezwe pia kwa viongozi wa
kisiasa ili kunusuru watoto wa kike dhidi ya ukeketaji pamoja na ndoa
zautotoni.
Loliondo ndiyo inayoongoza kwa kufanya ukeketaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment