Serikali ya Uganda imeagiza kuanzia
sasa vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran vinavyoingizwa nchini humo vilipiwe
kodi.
Viongozi wa Kidini kutoka madhehebu
hayo mawili makubwa nchini humo wamepokea uamuzi huo kwa tahadhari kubwa na
mshangao huku wakisisitiza kwamba, vitabu hivyo vya kidini havipaswi kutozwa
kodi kwani vinatumika kujenga na kuimarisha imani za kiroho za wananchi wa
Uganda.
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la
Waislaam Nchini Uganda, Ramadhan Mugalu, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa,
hatua hiyo imevuka mipaka, na kuhoji inawezaje kutoza kodi neno la Mungu?
Kwa upande wake Kamishna wa Makanisa
nchini humo, Mchungaji Joram Kahenano, amesema Kanisa lake litalazimika
kuongeza bei ya Biblia moja kutoka shilingi za Uganda elfu tatu hadi elfu 18
ili kufidia gharama za kodi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily
Monitor, uamuzi huo umetolewa baada ya miezi kadhaa ya majadiliano kati ya
Mamlaka ya Kodi na Taasisi za Kidini.
Biblia na Qur'an Tukufu kutozwa kodi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment