Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi amesema kwamba hawataki Mwanasheria wa chama
chao, Tundu Lissu akirudi Tanzania awe mtu wa kuhudhuria kliniki
kwa ajili ya matibabu bali wanatarajia aingie kwenye 'struggle' moja kwa moja.
Ole Sosopi ameyasema hayo leo wakati
akijibu swali kwenye Kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kila siku ya Jumatano
kupitia ukurasa wa Facebook EATV, na kuongeza kwamba wanatarajia kiongozi
wao atarudi nchini mara tu atakapomaliza matibabu yake anayoendelea nayo huko
nchini Ubelgiji.
"Tundu Lissu tunataka
akirudi asirudi ku-atend clinic, aje aingie kwenye mapambano moja kwa moja.
Lissu ni kama kaka kwangu, alipopigwa risasi nilifadhaika sana, mpaka kesho
nawaza hawa watu walikuwa na dhamira gani" Ole Sosopi.
Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa
"Lissu ni 'asset' kwa Tanzania na Mungu amemponya kutuonyesha, na ndio
maana yupo mpaka leo".
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida
Mashariki na Mwanasheria wa Chadema alipigwa risasi na watu wasiojulikana
Septemba 7, 2017 alipokuwa kwenye maeneo ya nyumbani kwake Area D Jijini Dodoma
wakati alipokuwa akirejea kutoka katika majukumu yake.
Atakachofanya Lissu akirudi Tanzania chaanikwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment