Mugabe Ryoba
(23) aliyeolewa Nyumbantobu katika kijiji cha Merenga wilayani hapa Mkoa wa
Mara ameuawa kwa kukatwa na sime na mpenzi wake, Nchama Nchama (26) kutokana na
wivu wa mapenzi.
Akizungumzia tukio
hilo lililotokea jana mchana Mei 28, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma
Ndaki amesema baada ya tukio hilo, mtuhumiwa ametoroka.
“Matukio
ya watu kuuana kwa silaha za jadi zimeshamiri lazima hatua zichukuliwe
kudhibiti hali hii,”amesema.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Nyamieri, Dominick Kimoge amesema baada ya mwanaume kutoka
kwenye shughuli zake, hakumkuta Mugabe nyumbani na baada ya muda aliwasiri na
kuanza kumhoji akimtuhumu kuwa alikuwa kwa mwanaume mwingine.
Amesema
alimshambulia kwa fimbo na mwisho akamkata kwa sime mkono wa kulia na
kusababisha damu nyingi kuvuja na kumuacha ndani na kwenda kutafuta
pikipiki ili kumpeleka zahanati.
Amesema
mwanamke huyo alifariki dunia kabla ya kuanza kupata huduma ya kwanza, kwamba
mtuhumiwa huyo ametokomea kusikojulikana.
Julius
Magoiga mkazi wa kitongoji cha Mafyweko amesema “aliyekufa hakuwa mke wa
mtuhumiwa kwa kuwa aliolewa na mama mmoja Ryoba Kibisa (nyumbantobu). Mtuhumiwa
alikuwa ni kama dume la mbegu tu maana watoto wote wawili aliozaa hapo watakuwa
wa mama aliyetoa mahari.”
Amebainisha
kuwa kwa mila na desturi za wakurya akina mama ambao hawakuzaa watoto wa kiume
hulazimika kutafuta mwanamke na kumtolea mahari na anaweza kumchagulia mwanaume
au atakayejitokeza akipata watoto hubaki kama wajukuu wa mji huo.
Amuua mpenzi wake kwa wivu wa mapenzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment