Mwanasheria
maarufu nchini ambaye kwa sasa ndiye rais wa Tanganyika Law Society (TLS), Bi.
Fatma Karume, amesema kwamba hana mpango wa kuingia kwenye siasa, licha ya
kuonekana akikosoa sana wanasiasa na baadhi ya vitu vinavyofanywa na serikali.
Akizungumza kwenye
kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio, Fatma Karume amesema
hataki kuingia kwenye siasa kwa sababu anapenda kuwa huru, licha ya kwamba
hatoacha kuendelea kukosoa serikali na wanasiasa pale wanapokosea.
“I like my freedom,
napenda kufanya vile ninavyoona mimi, kama serikali inafanya vitu kinyume na
sheria nitasema kwamba hivi sio vizuri, si vizuri kuvunjia watu majumba yao
wakati kuna court order, nitasema sitaogopa, ila sitaki kugombea, sitaki siasa,
I like to be left alone”, amesema Fatma Karume.
Fatma Karume
ameendelea kusema kwamba kitendo cha kuonekana kuikosoa serikali mara kwa mara
na kutetea baadhi ya vyama vya siasa, anafanya hivyo kwa sababu haungi mkono
uvunjaji wa sheria kwa namna yoyote ile, iwe inafanywa na serikali au vyama vya
siasa.
"Siungi mkono
uvunjaji wa sheria hata ukiwa upande wowote, mimi ni mtu huru, kama kitu
hakiendi kwa mujibu wa sheria nitasema, sio kwamba unakosoa vitu una ugomvi wa
serikali, sijali", amesema Fatma Karume.
Sitaki Siasa – Fatma Karume
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment