Rais John Magufuli amezitaja changamoto nne
zinazoikabili Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwamo vikwazo vya kiuchumi
uwekezaji, ukosefu wa viwanda, kutoaminiana ndani ya jumuiya hiyo na ujenzi wa
miundombinu
Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 24,
alipokuwa akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (Eala) katika mkutano wake wa
nne kikao cha kwanza ulioanza jana mjini Dodoma ikiwa ni mara ya kwanza vikao
vya bunge hilo kufanyika mkoani humo. Pia ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli
kuhutubia bunge hilo
Amesema mbali na mafanikio, jumuiya hiyo
inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo migogoro ambaye amesema imegharimu
maisha ya watu wengi
Ametaja changamoto nyingine kuwa ni vikwazo
vya kibiashara na uwekezaji kuwa bado vipo na kutokuaminiana ndani ya wanachama
wa jumuiya hiyo
“Mara nyingi huwa hatupendi kuyasema sema
haya lakini mimi nayasema ili muyabebe na mjue hiyo chalenji, pamoja na
changamoto nyingine nyingi mnapaswa muanze kuzitoa mapema,” alisema Magufuli.
Rais Magufuli ataja changamoto za EAC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment