Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa jana amepangua hoja wa wabunge waliokuwa
wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo huku akithibitsha kuwa Serikali
inatarajia kununua ndege nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu.
Alisema Serikali haikurupuki kununua
ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na
wakati.
“Serikali itaendelea kununua ndege
na haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.
“Nia ya serikali ni nzuri kwani
huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna shirika lako la ndege, hivyo
tumenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na zinafanya kazi.
"Mwaka huu tunategemea ndege
tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa marefu yenye uwezo wa kuchukua
abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 132 kila moja ni
Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia na kuanza kufanya kazi.
“Kikawaida huwezi kuwa na ndege moja
ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo kwenye bajeti hii tumeshapanga
kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe na ndege mbili za masafa marefu
ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou na moja inatoka
Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio utaratibu unavyokwenda,” amesema.
Aidha, amesema kwamba Kampuni ya
Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli kwamba haina kama wabunge
walivyodai ambapo kila baada ya muda inabadilishwa kwani si msahafu hivyo
itabadilishwa kutokana na mahitaji ya soko.
Mbarawa Apangua Hoja za Wabunge....Asema Ndege Nyingine Kubwa ya 7 Itanunuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment