Muigizaji na
Mfanyabiashara, Wastara Juma amesema kwenye maisha yake mwanaume anayejutia
kuwa naye kwenye mahusiano ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma
kwani hakumjua vizuri kabla ya kukubali kufunga naye ndoa.
Akizungumza leo kwenye kipindi
cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya
Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, ambapo amesema kwamba
alikubali kufunga ndoa na mwanaume huyo pasipo kumjua ni mtu wa aina gani.
"Najuta kuwa na mahusiano
na Sadifa kwa sababu sikuwa namjua vizuri. Tulifunga ndoa baada ya kujuana kwa
kipindi cha wiki moja. Alikuja kwa njia ya kunipa faraja kwa vile mimi ni
yatima, pia mjane lakini pia ni mlemavu. Mtu mimi akiniambia kitu kama hicho
anaweza kuiteka akili yangu kabisa," Wastara.
Hata hivyo Muogizaji huyo amesema
kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe
huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha
alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha
zote na Bunge.
Wastara ajutia ndoa yake na Mbunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment