WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara
kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa
kununua korosho kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho
alichokikuta ghalani.
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
“Tandahimba korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu
zinatoka wapi? Kuna kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini
walioleta korosho chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za
kisheria.”
Amesema haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza
alafu anakuja anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha
wasakwe.
Awali,
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms, ambapo
ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine mpya na kuanza
uzalishaji.
Hata hivyo amewataka wamiliki wa viwanda vyote vya kubangulia
korosho washirikiane na Serikali katika kufuata utaratibu wa kununua korosho.
Pia Waziri Mkuu amezindua barabara yenye urefu kilomita tatu
iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo imegharimu sh. bilioni 1.38
zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
Kwa
upande wake Meneja wa Kiwanda hicho Kwa Mahmoud Sinani alisema korosho
zinazobanguliwa kiwandani hapo zinauzwa ndani na nje ya nchi.
Amesema katika awamu ya kwanza ya uwekezaji huo umegharimu sh.
bilioni 12 na wanatarajia kuendelea na awamu ya pili ambapo watawekeza dola
milioni 20.
Amesema kwa sasa kiwanda hicho kimeajiri watumishi 250 na
wanatarajia kuajiri watumishi 1,500 mara baada ya kumaliza awamu ya pili ya
upanuzi wa kiwanda.
Pia Waziri Mkuu amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya wilaya
ya Tandahimba kwa kuweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombini ya barabara
kwa kiwango cha lami.
Viongozi Mtwara watakiwa kufuatilia watu wanaotaka kuharibu masoko ya korosh
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment