UMOJA WA WANAWAKE UWT MKOA WA ARUSHA WATOA MAFUNZO MBALIMABLI KWA WANAWAKE



Mwenyekit wa umoja wa wanawake UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akiwa na mjumbe wa baraza kuu taifa Ana Msuya ,Katibu wa UWT wilaya ya Arumeru pamoja na mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Arumeru

Aliyesimama ni katibu wa wanawake mkoa wa Arusha Bi Fatma akisisitiza jambo na walioketi ni viongozi wa wanawake Arusha pamoja na mwenyekiti wa UWT 
Wanawake wawakilishi katika baraza la wanawake wilaya ya Arumeru na watumishi wa serikali wakisiliza hoja mbalimbali katika ukumbi wa ccm Mkoa wa Arusha

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha akivalishwa kitenge kama zawadi aliopewa na wanawake wa baraza hilo wilaya ya Arumeru 


                                     Wanawake wa uwt wilaya ya Arumeru Arusha                                   kwenye ukumbi wa ccm mkoa wa Arusha

Mwenyekit wa umoja wa wanawake UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu amewataka wanawake wa jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyokuwepo kipindi cha uchaguzi na kushirikiana kwa pamoja ili kujenga chama na jumuiya hiyo.

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo kwa mara ya kwanza katika baraza la wanawake wa wilaya ya Arumeru ambalo limehusisha viongozi wa kata na matawi yote wilayani humo tofauti na viongozi wengine waliopita waliokuwa wanakutana na viongozi wa kata pekee yao.

Bachu pamoja na kuwataka wanawake kuvunja makundi kuanzia ngazi ya mkoa mpaka kwenye matawi katika wilaya ya Arumeru pia ameishukuru jumuiya hiyo kwa kumchangua kwa kura nyingi ambazo zimemuwezesha kupata nafasi hiyo.

                                  
Pamoja na hayo amesema kuwa kwasasa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kuendelea kushirikiana na amewakaribisha wenzake wawili ambao aligombea nao katika nafasi hiyo na kuwataka kushirikiana kwa pamoja kwa kuwa jukumu kubwa ni kuhakikisha wanaisimamia serikali na kushinda chaguzi zijazo.

“Kwa hiyo nawaomba kwa dhati ya moyo wangu kama kiongozi wenu mkuu kwenye ngazi ya mkoa wakina mama kuanzia kwenye tawi,kata ,wilaya vunjeni makundi ondoeni tofauti zenu malizeni kabisa kama kuna mahala pana shida zaidi uongozi wa wilaya unakuja amesema mwenyekiti anaanza ziara tarehe 20 mwezi wa tatu kule muweke mambo yenu yale yalioshindikana msiache mwenyekiti akaja akapita mkabaki nalo halafu akiondoka mnasema aah tumeamua tu tunanyamaze hamtamaliza miaka 5
itapita sawa akina mama nimesema niliseme hilo kwa msisitizo kwasababu bila umoja wetu ushindi haupo”Alisema Bachu

“Uongozi huu ni mpya kabisa na ni mpya kuanzia kwenu mpaka kwenye ngazi ya mkoa tunawathamini tunawajali sana wakina mama wote usipojali viongozi wa chini kabisa je wale wananchi wa kawaida wakinamama ambao bado hawajajiunga ccm bado hawajajiunga kwenye jumuiya lakini ni wapiga kura wameandikishwa  utawapataje hao na tunawategemea viongozi
wa matawi ndiyo mkatuletee wale ambao kesho na kesho kutwa tutakuja huko tuseme jamani mwenyekiti wangapi wameandikishwa kupiga kura hapa ambao wana shahada zao tuje tuwaombe kura sasa wewe mwenyewe kama ulikuwa mafichoni ili utuletee wale wapiga kura ndiyo mana tunasema tumeanza upya”Alisema Bachu

Naye mjumbe wa halmashuri kuu Bi Anna Agatha Msuya amesema kuwa kinachogaribu Mkoa wa Arusha ni suala la makundi yaliyoko katika chama cha Mapinduzi ndiyo mana mpaka leo wanaongozwa na upinzani.

“Na niwasisitize tuache makundi arusha kinatugaribu makundi ukimtaka flani asipokuwa unaenda kumtengenezea fitna,Fitna hizo ndiyo zimetupelekea mpaka leo tunaongozwa na upinzani ,wapinzani wenyewe tumewatengeze sisi sasa tusipotubu sisi wote tumekubaliana mkoa wa Arusha tumependelewa tuko wanec sita tumemuahidi Mh Raisi Arusha tutaikomboa na hatutaikomboa wenyewe tutaikomboa na ninyi has wanawake
tujifungeni mikanda tuacheni chuki binafsi ukipigwa wewe leo amka simama endelea na kazi Ukitengenezewa zengwe amka fanya kazi kwasababu Bila Yesu msalabani alidhalilishwa sana lakini leo ndiyo tumekombolewa ni kweli si kweli “Alisema Ana Msuya

Naye katibu wa jumuiya hiyo ya wanawake Bi Fatma amesema kuwa katika
wilaya ya Arumeru idadi ya wanachama wa jumuiya ya UWT kwa mwaka 2017 walikuwa 5824 lakini kwa mwaka huu wameongeza wanachama 243 na kufikia sasa wanachama 6067 ambao amewahamasisha kuendelea kulipa ada kunzia ngazi ya tawi ili kuboresha jumuiya hiyo.

Katika baraza hilo pia wanawake hao wa Arumeru walipata fursa ya kupata mafunzo ya elimu ya ujasiriamali kwenye vikundi , mafunzo ya Sheria ya ndoa ,ardhi,miradhi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni muendelezo wa mabaraza kwa mkoa wa Arusha ambapo siku ya jumanne baraza kama hilo litafanyikia katika wilaya ya Meru.

UMOJA WA WANAWAKE UWT MKOA WA ARUSHA WATOA MAFUNZO MBALIMABLI KWA WANAWAKE UMOJA WA WANAWAKE UWT MKOA WA ARUSHA WATOA MAFUNZO MBALIMABLI KWA WANAWAKE Reviewed by KUSAGANEWS on March 19, 2018 Rating: 5

No comments: