Klabu ya Real Sociedad, imemfukuza kazi kocha wake Eusebio
Sacristan, baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa muda miaka miwili na nusu.
Eusebio amefukuzwa mwisho wa wiki iliyopita kufuatia kupoteza
mchezo dhidi ya Getafe nyumbani kwa bao 2-1 na kuiacha Real Sociedad katika
nafasi ya 15, na pointi 33 baada ya kucheza michezo 29 ikiwa ni nafasi mbaya
kukamata klabu hiyo tangu msimu wa mwaka 2011-2012.
Aidha, Kocha huyo wa zamani wa kikosi cha pili cha Barcelona
alijiunga na klabu hiyo kuchukua nafasi ya David Moyes, Novemba 2015, na
kuisimamia kwa michezo 112, huku msimu uliopita akiiongoza timu hiyo
kufunzu mashindano ya kombe la shirikisho barani ulaya baada ya kumaliza katika
nafasi ya sita kwenye ligi ya Hispania,La liga.
Wakati huo huo,Klabu hiyo imemtangaza kocha wa kikosi cha pili
Imanol Alguacil kuwa kocha wa muda ambaye ataifundisha Sociedad mpaka mwisho wa
msimu.
Real Sociedad yamtimua kocha wake.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment