POLISI WAVAMIA MSIBA MWINGINE

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limevamia msiba mwingine na kuwafurusha waombolezaji kwa silaha za moto kwa madai kuwa viongozi wa Chadema wanatumia misiba ya wafuasi wao kufanya vikao vya siri vya kisiasa.

Kitendo cha polisi kuvamia msiba huo na kufurusha waombolezaji kimeongeza uchungu kwa familia iliyofikwa na msiba, huku mjane wa marehemu akilia hadi kupoteza fahamu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Ahmed Msangi amesema zoezi la kuwafurusha wafuasi wa Chadema wanaotumia misiba kufanya siasa ni endelevu, huku akionya waombolezaji watakaojaribu kuzuia polisi kufanya kazi yao, na kwamba ikitokea hivyo Polisi watatumia nguvu kuwafurusha.!

POLISI WAVAMIA MSIBA MWINGINE POLISI WAVAMIA MSIBA MWINGINE Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: