Waziri wa Viwanda,
Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa hapendezwi na bei elekezi za
sukari zilizopo kwa sasa na anajitahidi kutengeneza viwanda vidogo vya sukari
kama 100 ili soko la sukari lijiendeshe lenyewe.
Amesema hayo katika ziara yake ya
kushtukiza mkoani Manyara na kuweza kutembelea kiwanda kidogo cha sukari cha
Manyara Sugar na kuona uzalishaji uliopo na kusema kuwa kupanda kwa bei
nikutokana na viwanda vingi kufungwa lakini serikali imetoa vibali vya kuagiza
tani mia moja thelathini elfu na kwa sasa zimeshaanza kuingia na mpaka mwezi
wa sita zitazuiliwa ikiwa tayari viwanda vya ndani vitaanza kusambaza sukari
hiyo.
Pamoja na hayo Waziri Mwijage
amefungua eneo maalumu la ujenzi wa viwanda ambalo linaukubwa wa ekari 9.14
ambapo ekari 6.855 litajengwa majengo matatu ambayo yataanzishwa viwanda kumi
vidogo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kiwanda cha Manyara Sugar BW. Bharabat Sesodya amesema kuwa kutotosheleza kwa
sukari ni kutokana na udogo wa uzalishaji lakini kwa sababu mwaka huu wanamiwa
ya kutosha lazima wafikie lile lengo la serikali lililo kusudia.
Mwijage achukizwa na Bei ya Sukari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment