MWENYEKITI WA MTAA MIKONONI MWA TAKUKURU KWA KUTOZA FEDHA WANACHI ILI KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA NIDA
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlimani Kata ya Muriet Jijini Arusha Bwana Yohana Gasper
amekamatwa na Tasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Takukuru kwa kuwatoza wananchi fedha za usajili wa uandikishaji wa Vitambulisho NIDA.
Akizungumza na Wandishi wa habari kaimu mkuu wa TAKUKURUKU Mkoa wa Arusha Frida Wekesi amesema kuwa mwenyekiti huyo alikuwa akiwataka wananchi kutoa kiasi cha Shilingi 2000 kwa ajili ya Kujaziwa fomu ili waweze kupata vitambulisho vya taifa hasa wale wasiojua kusoma na Kuandika na wasioweza kujaza fomu hizo.
Frida amesema baada ya kupokea malalamiko toka kwa wananchi maafisa wa takukuru walifuatilia na kumkuta Mwenyekiri akiwa anafanya zoezi hilo la ujazaji wa fomu ndipo maafisa wa takukuru wakajichanganya kama wananchi wa kawaida ndipo wakabaini ukweli huo.
Maafisa hao walishuhudia wananchi wakichangishwa shilingi 300 kwa ajili ya kupewa fomu namba 7 ambayo ilitakiwa kujazwa na mwananchi ambaye hana kitambulisho cha mpiga kura na bima mbalimbali na katika zoezi hilo alikuwa akishirikana na vijana wawili ambao wote walikamatwa.
Hata hivyo maafisa hao wa Takukuru baadae waliwasiliana na na mtendaji wa kata afisa usajili wa NIDA wakafika eneo hilo na kutoa elimu kuwa mwananchi anayesajiliwa ili kupata kitambulisho cha NIDA hapaswi kutozwa pesa yeyote ambapo mwentekiti huyo alirudisha fedha hizo jumla ya Shilingi 56,000 alizokuwa amewatoza wananchi kwa ajili ya Vitambulisho.
Hata hivyo mwenyekiti huyo ameachiwa kwa Dhamana jana tarehe 13 /03 2018 wakati uchunguzi ukiendelea.
Vile vile Takukuru wamewataka baadhi ya viongozi kuacha tabia ya kuwadhulumu wananchi haki zao za msingi na wawe na huruma kwa wapiga kura wao na kuwavunja moyo wananchi wanaotaka Vitambulisho ambavyo ni haki yao kuvipata Bure.

Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment