UKIAMBIWA Mombasa raha, usibishane kwa kuwa kuingia huko ni rahisi, kutoka yumkini huwa vigumu kwa kuwa ukiwa na ngawira, anasa na majivuno hutawala katika mji huu mkongwe zaidi nchini Kenya.
Mmoja wa watalii wa kwanza katika Mji huu alikuwa ni Ibn Battuta wa Morocco mwaka wa 1331; naye mtalii mwingine kutoka Uchina, ni Zheng He aliyezuru mji huu mwaka wa 1413.
Huu ndiyo mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya Nairobi.
Idadi ya watu Mjini humo inakisiwa kuwa milioni mbili, wakijumuika ndani yake makabila karibu yote ya hapa nchini na raia wa kigeni pia.
Mji huu ndiyo makao makuu ya Kaunti ya Mombasa na ambapo gavana wa sasa akihudumu kwa awamu ya pili ni Hassan Joho - ni mwingi wa mengi ya siasa za kujitambulisha kama mfaafu zaidi kuwa Sultani wa Karne ya 21 wa Mombasa. Kwa mashauo humwezi.
Mji wa kitamaduni, huwa unazua hisia za ukiukaji haki za kibinadamu kwa kuwa biashara ya ulanguzi wa watu ishawahi kushirikishwa hapa.
Mji wa kitalii, ni mji ambao ni hifadhi ya bahari la Kihindi na ni wa manufaa sana kwa mengi ya mataiofa ya kigeni kufuatia usajali wake mwafaka katika ramani ya ulimwengu.
Ramani yake itakuonyesha ni Mji unaounganisha maeneo muhimu sana katika kuunda Mombasa kwa kuwa Mji wenyewe ni kisiwa; kikiunganishwa kushikamana na bonde la Tudor na Reitz na kuwa na kitovu Kilindini.
Kisiwa hicho kinaunganishwa na maeneo mengine kavu na daraja la Nyali, Feri ya Likoni na njia kuu ya Makupa. Kando ni reli ya kutoka Kenya hadi Uganda na kuna uwanja wa kimataifa wa ndege wa Moi.
Jamii zinazoweza kusemwa ni asili katika Mji huu ni Waswahili na Mijikenda lakini hali hiyo ikiendelea kuangamia kwa kasi kupitia kuingiwa na wengine wengi.
Historia ya Mji huu haina uwiano kwa kuwa wengine husema kuwa ulikuweko katika miaka ya 1150.
Vasco Da Gama ambaye husomwa kwa upana katika historia ya utalii anasemwa kuwa alitua katika mji huu mwaka wa 1498, Pedro Alvares Cabral akitembea mwaka wa 1500 huku Joao da Nova akitua mwaka wa 1505.
Afonso de Albuquerque alifika mwaka wa 1507.
Mji huu katika siku hizo za kujiweka katika ramani ya kitaifa ulikuwa ukifahamika kama Manbaça or Manbasa mwaka wa 1502.
Manbasa ini jina la Kiarabu kumaanisha 'Vita' kwa Kiswahili.
Ngome ya vita
Shehe Mvita ndiye hurejelewa kama baba mwanzilishi wa Mji huu na jina hilo la kivita lina uhusiano na mji huu kuwa ngome ya vita vya Kisiwa.
Jina hilo la Manmbasa/Manmbasa linafuatiliwa hadi ndani ya Quran, katika Surah Al Waqiah, 56: 6, kumaanisha kusambaratika, husiano ikiwa ni vita.
Ni mji uliotawaliwa na uingereza kati ya 1824 na 1826, kabla ya Sultan wa Zanzibar kuukodisha kwa kwa serikali hiyo ya kikoloni mwaka wa 1895 baada ya maafikiano ya mwaka wa 1885.
Ukawa ndiyo mji mkuu wa Kenya katika enzi hizo kati ya 1887 na 1906 kabla ya uhamisho kutekelezwa hadi Nairobi mwaka wa 1906.
Ufalme wa kuanza Mombasa unahusishwa na ma-sultan wawili— Mwana Mkisi na Shehe Mvita.
Mkisi hutajwa kwamba ni miongoni mwa akina babu wa Wapwani na ndiye alizindua eneo la Kongowea.
Shehe Mvita naye alishiriki vita vya ukombozi kutoka kwa Mwana Mkisi na akageuza Mji huo kuwa wa Kiislamu ambapo alianza kwa kujenga Msikiti wa Kisiwa cha Mombasa ukiitwa Mnara, mwaka wa 1300.
Mji unaohusishwa na uzinduzi wa biashara za kimataifa, katika biashara halali na haramu.
Wareno nao walitwaa mji huu kabla ya Waingereza mwaka wa 1589 na ambapo miaka minne baadaye walijenga mnara wa Fort Jesus kama makao ya kiutawala.
Kulizuka vita mwaka wa 1631 vikiongozwa na Dom, vita vilivyoishia kuchinjwa kwa wanajeshi wa Ureno lakini aliishia kutoweka na mwaka wa 1632, utawala wa Ureno dhidi ya Mombasa ukarejea mamlakani.
Sultan wa Oman alitwaa mji huu mwaka wa 1698.
Ni mji ambao katika historia hakuna uwiano kamwe lakini cha maana kuishia kujua ni kwamba, ni mji wa taifa huru la Kenya na ambao una manufaa tele katika maisha ya kibiashara, kijamii na kisiasa.
Mji ambao dini kuu ni Uislamu, katika siku za hivi karibuni umekuwa ukiangaziwa sana katika visa vya kuhifadhi bioashara ya mihadarati, kuhifadhi was

Mombasa ndiyo mji wa Maraha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment