Mahakama Kuu yamtaka DCI, IGP, NA MWANASHERIA MKUU KUMPELEKA ABDUL NONDO MAHAKAMANI

Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa wito kwa Mkurugenzi wa Upelelezi Tanzania (DCI), Mkuu wa Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani hapo kujibu hoja kuhusu Nondo kutofikishwa mahakamani.

Akizungumza  Wakili wa kujitegemea, Jebrah Kambole amesema wamewasilisha maombi kuhusu Nondo katika Mahakama hiyo tangu Ijumaa iliyopita wakiwa na hoja tatu.

Amesema maombi hayo wanaomba apewe dhamana, ama apelekwe mahakamani ama aachiwe huru.

“Tangu aletewe Dar es Salaam hakuna aliyeonana naye si ndugu, mawakili wala wanafunzi wenzake na hajafikishwa mahakamani hivyo tumeona njia ya pekee ni kwenda mahakamani kwa sababu ana haki ya kupata dhamana kama watu wengine,”-Jebrah.

Jebra amesema kuwa kutokana na maombi waliyoyafungua, leo March 19, Mahakama Kuu imetoa wito kwa DCI, IGP na AG ili wafike mahakamani kujibu hoja hizo.

“Mahakama imetoa wito kwa viongozi hao ambapo wametakiwa kufika mahakamani March 21, 2018,” -Jebrah
Mahakama Kuu yamtaka DCI, IGP, NA MWANASHERIA MKUU KUMPELEKA ABDUL NONDO MAHAKAMANI Mahakama Kuu yamtaka DCI, IGP, NA MWANASHERIA MKUU KUMPELEKA ABDUL NONDO MAHAKAMANI Reviewed by KUSAGANEWS on March 19, 2018 Rating: 5

No comments: