JIJI LA ARUSHA LAKABIDHIWA GARI KWA AJILI YA KUTUMIKA KWENYE SEKTA YA ELIMU MSINGI

Gari lililokabidhiwa na Shirika la Ithemba kwa jili la Arusha kutumika upande wa elimu Shule za msingi


Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bwana Athumani Kihamia akiwa ndani ya gari kulijakiki kwa ajili ya matumizi walilokabidhiwa na shirika la Ithemba kwa ajili ya kusaidia shukle za msingi
Halmashauri ya jiji la Arusha lmekabidhiwa gari lenye thamani ya Shilingi Milioni 26 na shirika la Ithemba Foundation kwa ajili ya Kutoa huduma ya kusimamia shule za msingi na kufuatili mendeleo shuleni pamojana ukaguzi kwa upande wa shule hizo.

Wakikakibidhi gari hilo Mr Miguel na Madam Jack kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha Bwana Athumani Kihamia wamesema kuwa wana furaha kutoa gari hilo ambalo litamrahisishia kazi afisa elimu msingi kufika kwa wakati kutika maeneo ya shule ili kutatua changamoto za kielimu ili zifanye vizuri katika taaluma.

Akizungumza Mr Miguel amesema kuwa anaamini baada ya kutoa usafiri huo kwa afisa elimu ufaulu nao utakuwa mzuri tofauti na ilivyo hivi sasa kwa kuwa awali changamoto ilikuwa ni usafiri ukilinganisha na  miundombinu iliyopo.

Baada ya kupokea gari Hilo aina ya Prado T 659 BAP Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia amesema kuwa gari hilo watalitumia kwa ajili ya kufuatili maendeleo shuleni ,ukaguzi pamoja na taaluma.
Kihamia amesema kuwa pia shirika hilo limejitolea vifaa kontena lililopo Nethaland kwa ajili ya kuja hapa nchini katika jiji la Arusha lenye vifaa kwa ajili ya kusaidia upande wa Elimu na wanafanya mchakato wa kuona ni jinsi gani litafika hapa nchini.

“Wiki mbili zinazokuja pia huko tunakoenda tunaenda barani Europa kwa ajili ya kwenda kuongea nao kubadilishana mawazo namna gani tunaweza kuimarisha shule zetu za msingi lakini pia tutaandika barua kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye kamishina wa wilaya naye atamuandikia Kamishna wa TRA ili kurahisisha mambo yetu ya ushuru na nini kwasababu vile vifaa vinavyokuja kwa ajili ya Shule Kwahiyo mimi niseme ninawashukuru sana na tunawaomba kila mnapopata nafasi hii muweze kutusaidia tena Thank you Very Much”Alisema Kihamia

Naye kaimu afisa Elimu shule ya Msingi jiji la Arusha Bi Unice Tondi ameshukuru Shirika hilo kwa kutoa gari kwa kuwa awali walikuwa na gari moja ambapo walikuwa wanapata changamoto lakini baada ya kupata gari la pili utendaji kazi utakuwa rahisi zaidi tofauti na mwanzo na ufaulu utakuwa mzuri zaidi.

JIJI LA ARUSHA LAKABIDHIWA GARI KWA AJILI YA KUTUMIKA KWENYE SEKTA YA ELIMU MSINGI JIJI LA ARUSHA LAKABIDHIWA GARI KWA AJILI YA KUTUMIKA KWENYE SEKTA YA ELIMU MSINGI Reviewed by KUSAGANEWS on March 08, 2018 Rating: 5

No comments: