Jeshi la
Polisi mkoa wa Kipolisi Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa mwili
wa mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah , ambaye
alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo jana.
Akizungumza Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mara Jafari Mohamedi, amesema hapo jana walipata taarifa
kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye mwili ndani, na
walipokifungua na kuita watu kutambua, ndipo alipojulikana kuwa ni mwili wa
mfanya biashara huyo anayeishi mkoani Mwanza.
“Jana jioni tumeweza
kupata mwili wa marehemu huyu Samson Josiah ambaye ni mmiliki wa mabasi ya
Super Sammy anayeishi Mwanza, kwamba kuna mwili umeonekana katika mto ambao
unatenganisha mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu unaoelekea mbugani Serengeti,
wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa polisi
kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu, kwa sababu tulikuwa na taarifa za
utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na wakatambua
mwili wa marehemu”, amesema Kamanda Mohamedi.
Kamanda Mohamedi
aliendelea kwa kueleza kwamba marehemu alitoweka kuanzia tarehe 27 mwezi
wa pili ambapo aliondoka mkoani mwanza, na ndugu zake walisema kuwa aliaga
anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara na kuna mtu anamdai na akapotea
tangu siku hiyo, na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa mtoto
maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea kabisa.
Imeelezwa kwamba kwa
sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya
postmoterm, na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, na mpaka sasa watu wanne
wameshikiliwa kufuatia tukio hilo, upelelezi bado unaendelea
No comments:
Post a Comment