"Hatuelewi Lengo la Polisi wamekusudia kutufanyia kitu Gani"Mrema

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakielewi lengo la Jeshi la Polisi mpaka sasa limekusudia kuwafanyia kitu gani viongozi wa Chadema kwa madai wanaitwa kila uchao halafu hakuna kinachojadiliwa kuhusiana na wito wao.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema mchana wa leo (Machi 16, 2018) alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii baada ya kupita muda mchache tokea Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu kuhudhuria kituo cha Polisi Jijini Dar es Salaam kama walivyotakiwa hapo awali kufanya hivyo na mwishowe kuachiwa kurudi walipotoka bila ya kuhojiwa jambo lolote lile tangu walipofika hapo majira ya asubuhi.

"Ni kweli Mwenyekiti Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalim waliripoti Polisi lakini hakukuwa na majadiliano ya aina yeyote yaliweza kufanywa siku ya leo.  Hatujui mpaka sasa Jeshi la Polisi linatutakia nini, kwa maana ninavyojua watu wakisha chukuliwa maelezo huwa Polisi wanaangalia kama watakuwa na kesi ya kujibu au laa, na kama itakuwepo basi wanapelekwa Mahakamani na kama hakuna basi jalada linafungwa. Sasa kwa upande wetu Jeshi la Polisi halijafunga jalada wanasema bado uchunguzi unaendelea", amesema Mrema.

Pamoja na hayo, John Mrema ameendelea kwa kusema "kwa kweli sisi mpaka sasa hivi tunaona ni usumbufu na hii sio mara ya kwanza maaana hata Mhe. Edward Low
"Hatuelewi Lengo la Polisi wamekusudia kutufanyia kitu Gani"Mrema "Hatuelewi Lengo la  Polisi  wamekusudia  kutufanyia  kitu  Gani"Mrema Reviewed by KUSAGANEWS on March 16, 2018 Rating: 5

No comments: