Miwani za urembo maarufu
kama miwani za jua zimetajwa kuwa na madhara kwa watumiaji wake kutokana na
watu kutofahamu saizi za namba ambazo wanapaswa kuzivaa kabla ya kununua.
Akifafanua kwenye kipindi cha
Supamix kinachorushwa East Africa Redio, Daktari Ningwa wa Upasuaji wa
macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk.Neema Daniel Kanyaro amesema
watu wengi amekuwa wakivaa miwani pasipokjua kwamba zinaweza kuwasababishia matatizo
ya kuona.
Dk. Kanyaro amesema kwamba watu
wamekuwa wakivaa miwani za jua kama urembo pasipo kwenda kupima kujua ni aina
gani ya miwani wanazotakiwa kuzitumia lakini pia bila kujua kama miwani hizo
zina namba ambazo kila mtu ana namba kutokana na uono wake.
"Miwani ni dawa lakini usivae
bila kupima kwani inaweza kukusababishia matatizo ikiwemo uoni hafifu. Unaweza
kukuta unavaa miweani nyeusi lakini kumbe siyo namba yako. Kama hujijui unaweza
kuta ukitazama unaona giza kumbe umeshaua macho kwa urembo" amesema.
Akizungumzia kuhsu presha ya macho
Dk. Kanyaro amesema kwamba ugonjwa huo hauna dalili za moja kwa moja bali ni
lazima kupima na huathiri watu wa rika zote.
Dk. ataja athari za miwani ya urembo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment