Diwani Mwingine wa NCCR aelekea CCM

Aliyekuwa Diwani kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Laurent Poteza, amejivua nyazifa zake zote ndani ya chama hicho na kujiunga CCM na kusema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli.

Akizungunza katika baraza la Halmashauri Kuu ya wilaya ya Kasulu Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Hamphrey Polepole amesema ameamua kujiunga na CCM ili kuungana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuijenga nchi.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Hamphrey Polepole kwa sasa yupo katika mkoa wa Kigoma na inadaiwa atakuwepo huko kwa muda wa mwezi mzima katika kujenga chama chake cha CCM.
Diwani Mwingine wa NCCR aelekea CCM Diwani Mwingine wa NCCR aelekea CCM Reviewed by KUSAGANEWS on March 16, 2018 Rating: 5

No comments: