Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Tamisemi, Selemani Jafo, amesema jumla ya wanafunzi
650,862 ambao sawa na asilimia 98.31, wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na
masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma, Waziri Jafo amesema wanafunzi wengine 11,173 ambao ni sawa na
asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakuweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza katika awamu hiyo kutokana na uhaba wa miundombinu.
Amesema idadi ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu imeongezeka kwa 124,209 likiwa ongezeko
la asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya
kwanza mwaka huu.
Aidha, amesema baadhi ya wanafunzi
wa mikoa ya Lindi, Mbeya, Rukwa, Manyara, Katavi na Simiyu, wamekosa nafasi
kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu katika mikoa yao vikiwemo vyumba vya
madarasa.
Wanafunzi 650,862 wachaguliwa kidato cha kwanza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment